Habari za Punde

Serikali itaendelea kuimarisha viwanja vya michezo ili kuibua vipaji vya vijana Nchini.

Serikali itaendelea kuimarisha viwanja vya michezo ili kuibua vipaji vya vijana Nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita wakati alipofanya ziara ya kukaguwa maendeleo ya  ujenzi wa Viwanja vya  Kitope Sports Complex Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema Ujenzi wa viwanja hivyo ni miongoni mwa ujenzi wa viwanja 18, vinavyojengwa katika Wilaya na Mikoa hivyo aliwashajihisha wakandarasi hao kuengeza nguvu ili kumaliza kwa wakati.

Aidha Mhe. Tabia, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa miongozo madhubuti anayoitoa katika kuwatumikia Wananchi wake.

Nae Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame amesema ujenzi wa viwanja hivyo imezingatia miundombinu bora kwa watu wenye mahitaji Maalum ili  waweze kupata fursa ya kuvitumia.

Aidha amewataka watumiaji wa Viwanja hivyo, kuwa waangalifu na kuvitunza ili viweze kufikia malengo yaliokusudiwa ya kutumika kwa muda mrefu.

Kwa Upande wake Mshauri elekezi Shadia Fauz Mohamed amesema mpaka sasa Mradi wa ujenzi wa viwanja hivyo unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Hata hivyo amesema kuwa, wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kunyesha Mvua jambo ambalo linazorotesha ujenzi wa viwanja hivyo.

Mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo Kitope Wilaya ya Kaskazini 'B' ambapo umejumuisha sehemu ya kubadilishia nguo, kiwanja cha mpira wa miguu, viwanja vidogo vidogo  vikijumuisha mpira wa mikono, mpira wa wavu pamoja na mpira wa kikapu. 






Imetolewa na Kitengo cha Habari, WHVUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.