Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AZINDUA TAWI LA BENK YA CRDB - BUHIGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela kwa kutambua mchango wa Benki hiyo katika maendeleo ya Wilaya ya Buhigwe wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Mabenki kubuni mipango mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa umma na kuelekeza nguvu zaidi katika kukuza uelewa juu ya masuala ya kifedha pamoja na umuhimu wa kutumia huduma za benki.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe mkoani Kigoma.  Amesema elimu na uelewa kuhusu masuala ya fedha umeonekana kuwa mdogo miongoni mwa wananchi kitu kinachopelekea baadhi yao  kushindwa kufahamu kuhusu bidhaa na huduma za kifedha zilizopo na ushirikiano uliopo kati ya watoa huduma za fedha na umma.

Ametoa rai ya kuendelea kuwapa wateja na wananchi wote kwa ujumla, elimu juu ya umuhimu wa kuweka akiba, kukopa na kurejesha na kutumia fedha walizokopa kwa malengo yaliyokusudiwa. Aidha amesema ni vema Wananchi waelimishwe umuhimu wa kuwa na akaunti benki ili fedha zao ziweze kuwa salama na wakifanya malipo kupitia benki wanajijengea historia nzuri ya kukopesheka.

Vilevile, Makamu wa Rais ameipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake katika kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Amesema kampeni shirikishi zinazotekelezwa na Benki hiyo zinatoa hamasa kwa wananchi na taasisi nyingine, ikiwemo sekta binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali katika uhifadhi wa mazingira.

 

Amewasisitiza kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana na Wana-Buhigwe katika kufadhili miradi ya kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema Wilaya hiyo yenye hazina kubwa ya uoto wa asili, inakabiliwa na tishio kubwa la athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Makamu wa Rais amesema mafanikio yaliyopatikana ni matokeo ya jitihada za Serikali kusimamia mageuzi makubwa na maboresho ya mazingira ya biashara, ili kuhakikisha sekta ya benki inakua na kuchangia kikamilifu katika uchumi wa Taifa. Amesema Serikali imeendelea kuwezesha ubunifu na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya fedha, hatua iliyozaa mafanikio makubwa, kama vile huduma za kibenki za kidijitali, huduma za fedha kupitia simu, huduma za kibenki mtandaoni, na pia huduma za uwekezaji kama vile Hatifungani ya Kijani, Hatifungani ya Miundombinu ya Samia na Hatifungani ya Sukuk.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe kuzindua Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe kuzindua Tawi la Benki ya CRDB Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua rasmi Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua rasmi Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buhigwe Bw. George Mbilinyi kuhusu ukarabati wa madarasa ya Shule ya Sekondari Kibande uliofanywa na Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe mara baada ya kuzindua tawi hilo katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpongeza mwananchi wa Buhigwe mwenye ulemavu  Bw. Adolf Ndamsanyi aliyekuwa mmoja ya wachangiaji wa fedha kwaajili ya ukarabati wa shule Wilayani Buhigwe wakati wa harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais katika uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 27 Agosti 2025.



 

Halikadhalika, Makamu wa Rais ameongeza kwamba, kupitia 


sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha na Mfumo wa 


Ujumuishi wa Kifedha, Serikali imejipanga kupunguza idadi 


ya Watanzania wasiofikiwa na huduma rasmi za kifedha, 


hususan vijijini. Aidha, Serikali inaendelea kuwekeza katika 


miundombinu ya TEHAMA, ikiwemo kuimarisha mkongo wa 


Taifa wa mawasiliano na kupunguza gharama za mawasiliano 


ili  kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kifedha za 


kidijitali kwa urahisi.


Makamu wa Rais ameishukuru Benki ya CRDB kwa ukarabati 


wa Shule ya Sekondari ya Kibande ikiwa ni madarasa mawili, 


ofisi ya Mkuu wa Shule, pamoja na upatikanaji wa viti na meza 


kwa ajili ya wanafunzi.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi waliojitolea kuchangia ukarabati wa Shule ya Sekondari Kilelema na Shule ya Msingi Mhinda zilizopo Wilayani Buhigwe kupitia harambee iliyobuniwa wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB – Buhigwe na kuwashirikisha wageni waalikwa na wananchi wa Wilaya ya Buhigwe. Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 246,684,000 zilipatikana ikiwa ni ahadi zilizotolewa pamoja na pesa taslimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela amesema Benki ya CRDB itaendelea kushirikiana na Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo ya ndani na nje ya nchi yenye kuleta tija na kukuza uchumi wa Tanzania.

Ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi na kukuza diplomasia ya kiuchumi iliyopelekea kuanzisha mradi reli ya Kisasa ya SGR kuelekea nchini Burundi. Amesema kupitia mradi huo, tayari Benki ya CRDB imetambua fursa iliyopo hivyo kujiandaa kuwawezesha wajasiriamali kuanzia wadogo hadi wakubwa ili waweze kutumia vema fursa hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amesema Wilaya hiyo itaendelea kushirikiana na Benki ya CRDB katika kuwaletea wananchi maendeleo, kwa kutambua kwamba maendeleo ya sekta yeyote, hutegemea sekta ya fedha ikiwa Benki ni muhimili mmojawapo wa sekta ya fedha.

Ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwekeza katika Wilaya hiyo ambayo kwa muda mrefu ilikosa matawi ya Benki. Amesema mwitikio wa wananchi kwa huduma za kibenki ni mzuri na wananufaika na bidhaa zitolewazo kwaajiili ya kujiimarisha kiuchumi na hivyo kuchagiza sekta zingine za uzalishaji na uchumi. Amesema kutokana jiographia ya Wilaya ya Buhigwe kupakana na Mataifa Jirani, Tawi hilo la Benki ni fursa kwa wananchi kibiashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.