Habari za Punde

OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA DMI WANDAA KONGAMANO LA UCHUMI WA BULUU

 

Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI) imeandaa kongamano la kitaifa la uchumi wa buluu ili kuwaleta pamoja wadau kujadili dira ya sekta hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2025, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi amesema kongamano hilo litawashirikisha washiriki zaidi ya 250 kutoka sekta za uchumi wa buluu za serikali, vyuo vikuu, vijana, wanawake na taasisi zisizo za kiserkali.

Alisema kufanyika kwa kongamano hilo ni utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Bluu (2024) ambayo inaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo imeweka dhamira ya kuhakikisha kuwa rasilimali bahari, maziwa na mito zinatumika kwa tija ili kuchangia kikamilifu uchumi wa taifa.

“Sote tunatambua kuwa uchumi wa buluu unaongeza ajira kwa vijana na kuboresha ustawi wa wananchi bila kuathiri mazingira,” alisema Mitawi.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Mitawi matarajio ya kongamano hilo ni kuziainisha fursa zilizopo katika sekta hiyo na kuonesha kwa namna gani zimebadili maisha ya wananchi na uchumi kwa ujumla.

Pia, alisema tayari Idara ya Uchumi wa Bluu imeanzishwa chini Ofsi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kuratibu sekta zinazohusika na uchumi wa buluu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.