Habari za Punde

WAZIRI PEMBE AHIMIZA AMANI WAKATI WA UCHAGUZ



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto MHE. RIZIKI PEMBE JUMA amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi kuimarisha Amani na usalama kuelekea uchaguzi mkuu 2025 ili uchaguzi huo ufanyike katika hali ya utulivu.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa Elimu kwa Mtandao wa Polisi Wanawake pamoja na kuwaaga Askairi wakike 27 wanaostaafu kazi, huko Ukumbi wa Chuo cha Polisi Zanzibar MHE. PEMBE amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha na kuendeleza Mtandao huo na amehimiza ushirikishwaji wa Askari wa kike katika kazi mbalimbali za Polisi ili kuleta usawa wa kijinsia.

Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. KOMBO KHAMIS KOMBO amewataka Askari wakike kuendeleza umoja na mshikamano ili kuimarisha Mtandao huo wa Polisi wanawake ambao umwekuwa ukileta tija kwa Jeshi Polisi na Jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) PILI FOBBE amesema lengo la kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi wanawake ni kuhamasisha haki na Jinsia ndani ya Jeshi la Polisi.

Kitengo cha Habari,

Makao Makuu ya Polisi

Kamisheni ya Zanzibar

Tarehe 27/08/2025


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.