Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameongoza Maziko ya Kaka Yake Marehemu Abass Ali Hassan Mwinyi Yaliyofanyika Kijijicha Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaongoza viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na mamia ya wananchi katika maziko ya kaka yake, marehemu Abbas Ali Mwinyi, aliyefariki jana.

Maziko hayo yamefanyika leo tarehe 26 Septemba 2025, katika Kijiji cha Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mapema, Dkt. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu, ndugu, jamaa na marafiki kwa Sala ya Ijumaa pamoja na Sala ya kumsalia marehemu katika Msikiti wa Jamia Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi.




 















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.