Habari za Punde

TAARIFA KWA UMMA TATHMINI YA OPERESHENI YA SIKU KUMI KWA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI

Mnamo tarehe 25/07/2025 hadi 04/08/2025 Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani(ZARTSA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), wamefanya operesheni ya pamoja ya siku kumi (10) katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Unguja. Katika Operesheni hio Jumla ya makosa 2,641 yalikamatwa. Gari zilikuwa ni 814 na pikipiki zilikuwa ni 1,827 na Tsh. 230,618,750/= zilitozwa kama Tozo kwa makosa hayo.

Katika kipindi hicho jumla ya ajali 03 za barabarani zililipotiwa zilizotokea katika maeneo ya Welezo na Mlandege kwa mkoa wa Mjini Magharibi na Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja. Katika ajali hizo jumla ya watu 05 walifariki na watu 04 walijeruhiwa.

Operesheni hiyo imeleta mafanikio makubwa kwani  imepunguza ajali za barabarani pia zimewafanya watumiaji wa vyombo vya usafiri barabarani kufuata sheria.

Aidha katika Operation hiyo pia yalikamatwa magari yaliyofunga namba zisizotambulika na Mamlaka za usajili kama SSH 25-30, MWINYI 2530, TAMBA NA AMEIR URAIS 2025-2023, kufunga taa za vimulimuli na baadhi ya magari kutumia nambari za Tanzania Bara bila ya kibali kutoka Mamlaka husika, vitendo hivi ni makosa kwa mujibu wa sheria ya Usafiri Barabarani ya Zanzibar.

Katika kipindi hicho cha siku kumi ulipaji wa Stika kwa magari ya Biashara pia uliongezeka jumla ya Tsh 80,000,000/= zililipwa ZRA na idadi ya vyombo vilivyopasishwa KWA SILVA viliongezeka.   

Pia zilikamatwa Pikipiki zisizo na nambari za usajili ambazo zimewekwa maneno mchanganyiko kama vile Wadudu, Mtukwao nk, kama ona hapa.

Wito kwa wananchi wote, Jeshi la Polisi linaendelea na Operesheni hiyo na tunawataka wananchi wote kuheshimu sheria za nchi na ataekwenda kinyume Jeshi la Polisi halitakuwa na muhali na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi wote wanaotaka kuweka namba au majina Binafsi wafuate utaratibu wa kwenda ZRA kusajili namba au majina hayo.

MAZOEZI YA PAMOJA YA VYOMBO VYA USALAMA

Mnamo tarehe 10/09/2025 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama wamefanya mazoezi ya pamoja ya kuweka utimamu wa mwili. Mazoezi haya ni kwamujibu wa taratibu na kanuni za uanzishwaji wa vyombo hivyo na yataendelea kufanyika. Wananchi wasiwe na khofu wala taharuki kwani vyombo viko timamu kwa ajili ya usalama wao.

Imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makossa ya Jinai, Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Zanzibar.

Tarehe 10/09/2025.


Imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makossa ya Jinai,

Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Zanzibar.

Tarehe 10/09/2025.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.