Na Mwajuma Juma
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi aliyemaliza muda Pandu Ameir Kificho leo anatarajiwa kuifungua Itikafu ya Kimataifa itakayofanyika huko katika Msikiti wa Said Washoto Welezo Wilaya ya Magharibi Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Itikafu, Khatib Twahir alilieleza hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa hizi huko Welezo wilayani ya Magharibi.
Alisema Itikafu hiyo itakuwa ya siku tisa au kumi itaaza majira ya saa 10:45 za jioni ambapo itajumuisha Waumini wa dini ya kiislamu zaidi ya 500, kutoka nchini mbali mbali za ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo alisema tayari baadhi ya Wawakilishi kutoka nchi zitakazoshiriki Itikafu hiyo wameshawasili ambapo wengine walitarajiwa kuingia mchana wa jana.
Twahir alitaja baadhi ya waumini waliokwisha wasili ni kutoka nchi za Burundi, Uganda, Zambia na Pemba, ambapo nchi zilizotarajiwa kuwasili jana ni Kenya, Malawi na Tanzania Bara.
Alifahamisha kwamba katika Itikafu hiyo zilitarajiwa kuwasili nchi 10 lakini kwa sasa hivi zitashiriki nchi nane baada ya Oman na Emirates kushindwa kuwasilisha washiriki wao.
Itikafu ya Kimataifa hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi 20 wa Ramadhan, ambapo katika kikao hicho waumini kupata fursa ya kusoma Hadithi, Qur'aan na kutoa Mawaidha.
Aidha pia hufanyika mashindano ya kuhifadhi Qur'aan na Hadithi za Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wasalam) kwa vijana waliochini ya umri wa miaka 16.
Mwenyekiti huyo alisema katika Itikafu ya mwaka huu, kiasi cha shilingi milioni 20 zinatarajiwa kutumika.

No comments:
Post a Comment