Habari za Punde

MDAU ANAHITAJI MSAADA WA MAWAZO UNAWEZA KUMSAIDIA?

Habari za kazi.
Mimi ni mtanzania ambae kwa sasa ninaishi Ureno katika mji mdogo wa Faro. Ninatatizo la Pasipoti. Nimepoteza Paspoti yangu na nimejaribu kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania uliopo Paris Ufaransa. Ila tatizo ni kuwa wananiambia lazima niende Ufaransa kushughulikia tatizo langu wakati mimi sina hati ya kusafiria na ikitokea kukamatwa itaweza kuniletea matatizo.
Sasa ninaomba msaada wa mawazo au rai kutoka kwa mtu yeyote na nitamshukuru sana ili niweze kupata Pasi nyengine haraka iwezekanavyo kitu gani nifanye? Nitawashukuru kwa mawazo yenu
Mdau kutoka Ureno. Email hikmma@live.com

1 comment:

  1. utaratibu ni kuwa ubalozi utume afisa wake aje huko kukuhudumia sio wewe kuufuata ubalozi. utasafiri vipi wakati huna pasipoti? jee hilo ni tamko la balozi au karani tu.

    mdau

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.