Zakaatul Fitr ni wajibu kwa kila Muislam awe mwanamke au mwanamme, mkubwa au mdogo, almuradi ana uwezo wa kuitoa au kutolewa kwa niaba yake ikiwa yuko anaemuangalia.
Muda wake ni tokea kutua kwa jua katika siku ya mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan mpaka wakati watu wanapotoka kwenda kusali sala ya Eid.
Hata hivyo Maulamaa wamekubaliana kwamba Zakaah hii inaweza kutangulizwa kabla ya muda wake kama walivyokuwa wakifanya Masahaba. Na hata kwa yule ambaye kwa njia moja au nyengine hakubahatika kutoa Zakaah katika muda wake bado anapaswa kutoa Sadaqa.
Asli yake hutolewa chakula kile ambacho ni maarufu katika mji/nchi na pia inajuzu kutolewa pesa kwa sharti kwamba kutakuwa na maslaha makubwa zaidi kwa anaepewa kuliko akipewa chakula au nafaka.
No comments:
Post a Comment