Hawa ndio tunaowatarajia kumpata mmoja ambae ndie atatangazwa kuwa mshindi na kuteuliwa Rais.
Kipima joto chetu kilichopo hapo pembeni kama kitaweza kutumika kama ndio mtazamo wa wapiga kura siku ya Jumapili kutokana na waliobahatika kutoa maoni yao kuhusu nani atakuwa Rais, basi tayari keshajulikana. Ila tu maoni haya yataakisi hali halisi kwenye vituturi? Tusubiri tuone. Blog yako inatanguliza shukrani za dhati kwa wote waliobahatika kutoa maoni yao
Iwe itakavyokuwa, ila mshindi siku ya Jumapili, InshaAllah ni wewe Mzanzibari utakayoitumia haki yako ya kupiga kura na kuchagua Viongozi katika ngazi zote ambao wataweza kuwa na upeo wa kuiongoza Zanzibar katika mfumo mpya wa umoja wa kitaifa.
Blog yako inawatakia kila la kheri na kuomba uchaguzi uwe huru, haki na wa amani uliojaa utulivu kama zilivyokuwa kampeni ambazo zimeuthibitishia ulimwengu kwamba kumbe tunaweza.
Nami kura yangu ni kwa...
Picha kwa hisani ya Chachandu blog, bashir-nkoromo.blogspot.com
Wa ukweli utamjuwa tu ana smile anafuraha Seif inshallah atashinda.
ReplyDelete