Habari za Punde

CCM YAHITIMISHA KAMPENI PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karuma, akiweka jiwe la msingi la barabara za Wete--Gando na Wete -- Konde, mbele jengo la Hoteli ya Wete Kisiwani Pemba jana. Kushoto Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said



WANACHAMA wa CCM Kisiwani Pemba, wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Dk. Ali Mohammed Shein, akitowa sera za chama chake katika mkutano wa ufungaji wa Kampeni za chama hicho kisiwani Pemba, uliofanyika kiwanja cha Gombani ya Kale Chake Chake jana



MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Shadya Karume na Mke wa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Mama Mwanamwema Shein, pamoja na Dk Maua Daftari wakicheza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kiwanja cha Gombani ya Kale jana.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, akiwahutubia wanachama wa CCM wa Mikoa miwili ya kisiwani Pemba, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM kisiwani Pemba, uliofanyika kiwanja cha Gombani ya Kale jana

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Ali Mohammed Shein, akizungumza na wanaCCM na wananchi waliofurika katika kiwanja cha Gombani ya kale, Chake Chake Pemba, kwenye mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho kwa CCM jana
KUTOKA kushoto Mama Shadya Karume, Mama Mwanamwema Shein, Maua Daftari na Mama Fatma Karume, wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM Pemba, Gombani ya kale jana
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, akiteta na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Ali Mohammed Shein, baada ya kumalizika mkutano

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.