Ni kujipatia amani, maendeleo zaidi
Rajab Mkasaba –Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, amewataka wananchi wa kisiwa cha Pemba kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM),ili kuendeleza maendeleo yaliopo pamoja na kuimarisha amani na utulivu.
Dk. Karume ambae ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, aliyasema hayo katika nyakati tafauti, alipokuwa katika ziara ya kikazi kisiwani Pemba jana.
Akiweka jiwe la msingi la barabara ya Wete-Gando na Wete-Konde, huko Bopwe, Rais Karume aliwataka wanachama, wapenzi wa CCM na wapenda amani, utulivu na maendeleo ya Zanzibar, kuwachagua wagombea wa CCM.
Aidha Dk. Karume aliwataka wanachama wa vyama vya upinzani ambao alisema anaamini wanapenda amani, utulivu na maendeleo kuwapa kura wagombea wa CCM, ili kuongeza kasi ya maendeleo na kufanikisha utendaji wa Serikali ya umoja wa kitaifa.
Rais Karume ambae aliwanadi wagombea wa nafasi za Urais kupitia CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa Urais wa Tanzania na Dk. Ali Mohammed Shein kwa Urais wa Zanzibar, pamoja na wagombea wote wa CCM kwa nafasi ya Uwakilishi na Madiwani na kusema wanayoahidi yote yanatekelezeka kama ilivyoelezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2010-2015.
“CCM tayari imeonesha uwezo wa kutekeleza kila inachoahidi na kina sera na ilani yenye kutekelezeka kama tulivyoshuhudia wenyewe kipindi kinachomalizika” alisema.
Pia Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM, aliwafahamisha wananchi wa Pemba umuhimu wa kuichagua CCM kwa vile inapoleta maendeleo haichagui tafauti ya vyama wala nyengine yoyote.
Akishangiriwa na umati uliojazana katika viwanja vya hoteli ya Wete, Dk. Karume, aliwataka wananchi hao kuelewa kuwa mipango ya maendeleo inafanyika hatua kwa hatua na kutaja mafanikio katika miradi ya miundombinu ya barabara na umeme, nchini kote, ikiwemo Pemba ambayo kwa muda mrefu ilikosa huduma hiyo kwa uhakika.
Akiweka jiwe la msingi Tawi la CCM, Makombeni, Mkoani Pemba, Rais Karume alisema, mtaji mkubwa wa chama hicho ni wanachama wake ambao ndiyo uhai na nguvu zake.
Dk. Karume alichangia bati la paa hilo, pamoja na fedha za kumalizia, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz, akichangia fedha za majengo ya kuezekea na malipo ya fundi bati.
Akizungumzia maendeleo ya wananchi wa Makombeni ambao amewaita kuwa ni wanamapinduzi halisi, Dk. Karume aliwaambia kujengwa kwa barabara ya lami ni njia moja ya kufungua milango ya maendeleo katika eneo hilo.
Rais Karume alimpongeza Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Maalum, Zainab Omar kwa kuchangia fedha nyingi za ujenzi wa Tawi hilo lililoanzishwa mwaka 1964 wakati wa ASP, pamoja na wote waliochangia kwa hali na mali.
Mapemba Dk. Karume aliwanadi Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo la Mkoani, Abdalla Abass (Mwakilishi), Issa Mohammed (Ubunge) na Samir Juma (Udiwani) kwa niaba ya Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa tiketi ya CCM kisiwani Pemba.
Mapema Rais Karume alipita Chonga, Mkoa wa Kusini Pemba kwa kuwafariji wafiwa na majeruhi ambao walipata ajali hivi karibu wakati wakirudi katika mkutano wa Kampeni wa CCM, uliofanyika Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aidha, wazee wa jamaa na ndugu wa majeruhi na wafiwa wa marehemu walitoa shukurani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kuwajali na kutoa misaada mbali mbali tokea siku iliyotokea ajali hiyo hadi leo hii.

No comments:
Post a Comment