Habari za Punde

JUMATATU NI SIKU YA 'ARAFAH

Assalaamu ‘Alaykum

Tunawatakia Waislamu wote waliobahatika kwenda Makkah kutekeleza ibada ya Hija Allah awatakabalie Hija zao, awaghufurulie madhambi yao na awapokee wageni wake kwa mikono iliyojaa kheri na tawfiyq InshaAllah.

Siku ya Jumatatu tarehe 9 dhulhajj 1431 ambayo inasadifu tarehe 15/11/2010 ni siku ya ‘Arafah. Mahujjaaj watakusanyika katika Mlima 'Arafah kwa ajili ya ibada kuu ya Hija. Ni Sunna iliyotiliwa mkazo kufunga siku hii kwa wasiobahatika kwenda Makka kuhiji. Kumbuka tunafunga SIKU ya ‘Arafah na si tarehe 9 kwa hivyo Waislamu wote inshaAllah tufunge Jumatatu kwani ndiyo siku ya ‘Arafah ambayo kwa kila mwenye kufunga husamehewa madhambi yake ya mwaka uliopita na uliopo.

Pia tuanze kujikumbusha kuhuisha na kurudisha Sunna zinazosahaulika kama Sunna ya kuchinja katika sikukuu hii kwa wote wenye uwezo kwani ni kuitikia Sunna ya Nabii Ibrahim ‘Alayhis Salaam.

Tunawatakia Waislamu wote Idd Mubaarak . Kila mwaka nyote mko katika kheri

2 comments:

  1. Salaam kaka, mbna rangi hii inaumiza macho km itawezekana usitumie tena coz we've to wear glass ili tupunguze mwanga, thnx kwa habari nimekua nikifuatilia blog yko takriban kila cku.
    God bless u

    ReplyDelete
  2. Thanks mdau na tayari tumebadilisha. Tunaomba radhi kwa usumbufu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.