Na Ali Mohamed, Maelezo
Benki ya Dunia (WB) imeahidi kufanaya kazi kwa karibu zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwawezesha wananchi kiuchumi hali itakayoimarisha maisha yao.
Akizungumza na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Mkurugenzi wa Benki ya duania kanda ya Afrika, John Murray aliitaka wizara hiyo kuandaa mapendekezo na kuyawasilisha katika benki hiyo.
Alisema benki ya dunia katika mpango huo inakusudia kutoa mafunzo maalum kwa wajasiriamali na wanavikundi ambapo hali itakayosaidia wajasiriamali hao kumudu kutumia rasilmali zilizopo kuboresha maisha yao.
Mkurugenzi huyo alieleza hayo kufuatia maombi ya Waziri wa wizara hiyo Haroun Ali Suleiman kwa benki hiyo kusaizadia Zanzibar juu ya suala la kuwawezesha wananchi na kuwainua kimaisha.
Aidha Mkurugenzi huyo alimpongeza Waziri Haroun kwa kuteuliwa kwake kuiongoza wizara hiyo ngumu lakini yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Nae Waziri Haroun aliishukuru benki ya dunia kupitia kwa Mkurugenzi huyo ambapo alisema kuwa ilimpa mashirikiano makubwa wakati alipokuwa waziri wa elimu.
Waziri Haroun alisema Wizara hiyo anayoiongoza ina jukumu kubwa la kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaishi katika maisha bora.
Wakati huo huo Mkurugenzi huyo alikutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdalla Shabaan kwa mazungumzo juu ya maendeleo ya mradi wa kuimarisha elimu ya lazima unaofadhiliwa na benki hiyo.
Katika mazungumzo hayo Waziri Shabaan alimfahamisha Mkurugenzi huyo kuwa mradi huo unaendelea vyema na kukamika kwa mradi huo sekta ya elimu itapata mafanikio zaidi.
Nae Mkurugenzi huyo alisema Benki ya Dunia itaendelea kuisadia Zanzibar katika miradi mbali mbali katika sekta ya elimu hasa kufuatia maelewano ya kisiasa yaliyopo nchini.
Mradi huo unajumuisha ujenzi wa skuli mpya 19, ukarabati wa skuli sita, ujenzi wa chuo cha walimu na kugharamia mafunzo ya walimu ambapo jumla ya dola za Kimarekani milioni 42 zitadumika katika mradi huo.
No comments:
Post a Comment