Habari za Punde

BENKI YA NBC ZANZIBAR YATOA MISAADA SKULI YA WATOTO MAUNGANI

 MENEJA wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar,  Rajab Maalim kushoto akimkabidhi kimoja ya viti vilivyotolewa na benki yake kwa ajili ya skuli ya Maungani wa Watoto wa Darasa la Chekechea Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Skuli hiyo Hassan Ali Mzee, makabidhiano hayo yamefanyika skulini hapo Maungani, Mkoa wa Magharibi Unguja. kulia Diwani wa Wadi ya Fuoni Shaka Hamdu na Afisa wa Benki hiyo Salama Abdalla.    
WAFANYAKAZI wa Benki ya NBC inavyoonekana wakisema hata na sisi tuvibonge viti hivi ndio wanavyoonekana wakipozi katika darasa lililokuwa na viti hivyo.
 MWENYEKITI wa Kamati ya Maendeleo ya Skuli ya Msingi ya Maungani, Hassan Ali Mzee akielezea wasifu wa skuli hiyo na jinsi wanavyosimamia, maendeleo ya watoto na kukuza elimu katika skuli hiyo wakati wa sherehe za kukabidhi madawati.
 DIWANI wa Wadi ya Fuoni Shaka Hamdu Shaka akitowa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar kwa msaada wao  na kujali jamii nini wanahitaji.   
 HATA na sisi tunataka kumbukumbu ya kutowa Msaada wa madawati na viti ndivyo inovyonekama mfanyakazi huyu akisema huku akichukuwa picha kwa njia ya simu yake.
 WAFANYAKAZI wa NBC Tawi la Zanzibar  wakimsikiliza Mkuu wao  akizungumza na Wazee na Wafanyakazi katika sherehe za kukabidhi madawati na viti kwa ajili ya Wanafunzi wa Chekechea wa Skuli ya Maungani.
  
 WAZEE wa Wanafunzi wa skuli ya Maungani wakimsikiliza Meneja wa Benki ya Biashara ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.