Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo kuhusu masuala ya teknolojia ya mawasiliano katika mtandao kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho.
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (wa kwanza kushoto) akikabidhi msaada wa kompyuta 10 zenye thamani ya shs milioni 12 zilizotolewa na Tigo kwa Chuo Kikuu cha Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita. Aliyepokea ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof Mustafa Roshash (wa tatu kushoto) na wengine wanaoshuhudia ni baadhi wa wanafunzi, walimu na wawakilishi wa Tigo.
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Tigo, imetoa msaada wa kompyuta 10 kwa Chuo Kikuu Zanzibar kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu katika chuo hicho.
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando, akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho mwishoni mwa wiki wakati wa kukabidhi zawadi hizo, alisema lengo la kampuni hiyo ni kusaidia serikali katika kuinua kiwango cha elimu nchini.
“Tigo inajisikia fahari kutoa zawadi hizi kwa Chuo Kikuu Zanzibar. Tunaamini mchango wetu utasaidia kubadilisha kiwango cha elimu kwa wanafunzi,” alisema Mmbando.
“Tunafahamu kuwa shule na vyuo vingi havina uwezo kumpatia kila mwanafunzi kompyuta, ingawa sasa mahitaji mengi ya shule yanahitaji matumizi ya kompyuta,” alisema.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Mustafa Roshash, msaada huo umetolewa wakati mwafaka wakati katika hatua za mwisho za kuanzisha kituo kitakachohitaji vifaa hivyo.
Aidha, Makamu Mkuu huyo alisema wanatarajia kufungua kitivo cha uhandisi hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment