Habari za Punde

SHEREHE ZA MUUNGANO MIAKA 47 ZAFANA UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk . Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Uwanja wa Amaan  akishindikizwa na Mapikipiki ya Polisi , katika kilele cha kutimia miaka 47 ya Muungano.  
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akipokea heshima ya wimbo wa Taifa alipowasili Uwanja wa Amaan  tayari kwa kukagua Gwarinde la heshima liliondaliwa  katika sherehe za Miaka 47 ya Muungano.  
VIONGOZI wa Serikali kutoka kushoto Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.  

ASKARI wa JW wakipita kabla ya kupita Rais kukaguwa  bwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama.  
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikaguwa Bwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama  katika maadhi,isho ya Sherehe za Miaka 47 ya Muungano.  
WANANCHI wakiwa katika majukwaa wakifuatilia maadhimisho ya sherehe za Muungano zilizofanyika Uwanja wa Amaan.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikaguwa Bwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika maadhi,isho ya Sherehe za Miaka 47 ya Muungano.





WAZIRI wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis Bakary na Waziri asiye kuwa na Wizara Maalum Suleiman Othman Nyanga  wakisoma magazine inayoonesha picha za  Muungano  wakiwa katika Uwanja wa Amaan.  
MAWAZIRI wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika Jukwaa maalum la Viongozi wakihudhuria  sherehe za miaka 47 ya Muungano Uwanja wa Amaan.
MWENYEKITI wa CUF Ibrahim Lipumba akihudhuria maadhimiso ya kilele cha sherehe za Muungano zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
HAWA ndio waliochukuwa chungu na mchanga uliochanganywa wakati wa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar kutoka kulia Hassan Omar, Sifaeli Shuma, Hassanieli Mrema na Khadija Abass Rashid, wakiwa katika moja ya Jukwaa Uwanja wa Amaan katika sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanzania. 
MABALOZI wanaowakilisha Nchi zao Tanzania wakiwa katika Uwanja wa Amaan wakihudhuria sherehe za Muungano kutimia miaka 47.
KIKOSI cha Bendera kikitowa heshima yake kwa Rais wa Tanzania katika kilele cha sherehe za Muungano zilizofanyika Uwanja wa Amaan.
GARDI ya Kwanza ikipita kwa mwendo wa pole mbele ya Rais wa Tanzania ikitowa heshima katika sherehe za kuadhimisha sherehe za Muungano Uwanja wa Amaan.

KIKOSI cha Anga kikitowa heshima yake kwa Rais wa Tanzania kwa mwendo wa polepole
KIKOSI cha Jeshi la Wanamaji kikitowa heshima  kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  
KIKOSI cha  Jeshi la Wananchi  Wanawake wakitowa heshima  kwa Rais wa Tanzania

HIVI ndivyo uilivyokuwa Wanajeshi wakirusha Mguu katika Bwaride la Sherehe za Muungano Uwanja wa Amaan
 KIKOSI cha Jeshi la Anga kikitowa heshima  kwa ukakamavu na kurusha mguu juu kuonesha umahiri wao wakipita kwa Rais wa Tanzania.
KIKOSI cha Askari Polisi wanawake nao walitowa burudani tosha kwa kurusha mguu wakipita kwa Rais wa Tanzania katika Maadhimisho ya sherehe za Muungano uwanja wa Amaan.




WANAFUNZI wa Skuli za Msingi wakicheza Halaiki katika maadhimisho ya sherehe za Muungano Uwanja wa Amaan.
Wanafunzi wa Skuli za Msingi wakicheza halaiki wakionesha alama ya Msumeno
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi ya Kimataifa ya Hazina kutoka Dar-es- Salaam  wakicheza Sarakasi katika sherehe za Maadhimisho ya MUUNGANO.  

WANAFUNZI  wacheza Halaiki wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kucheza halaiki katika sherehe za miaka 47 ya Muungano Uwanja wa Amaan.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao Tanzania katika viwanja vya Ikulu Zanzibar wakati wa tafrija ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Tanzania.  



RAIS wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Tanzania. 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha Nchi za Tanzania waliofika katika Viwanja vya Ikulu  kuhudhuria dhifa ya Chakula cha Mchana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Uturuki katika viwanja vya Ikulu wakati wa chakula cha Mchana.   
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi  Mbatia akifuatia Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba.     

RAIS wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Meya wa Mji wa Zanzibar Hatib Abrahaman Hatibu katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.