Habari za Punde

DK SHEIN ASHIRIKI MAZISHI YA MACHAPRALA

 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akishiriki na waumini wengine wa dini ya kiislamu kusalia Jeneza la marehemu Msanii Mzee Maulid Mohammed Machaprala, katika msikiti Nambar,Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.


 Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein,alishiriki  katika mazishi ya Msanii maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyefariki na kuzikwa jana kijijini Bambi,wilaya ya kati Unguja,pichani Dk  Shein,akitia udongo katika kaburi kama isharakatika mazishi hayo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,pichani na waislamu wengine wakishuhudia harakati za mazishi ya Msanii Maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyezikwa kijijini Bambi wilaya ya kati Unguja leo.


Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.