MFANYABIASHARA Mahmoud Kadhim Abass akikabidhi Mashine ya Fotokopi kwa niaba ya Familia ya Marehemu Sheraly Nisar Hussein ya Canada ambayo ina asili ya Zanzibar, kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Zanzibar Sichana Haji Fuom, ikitowa mashine hiyo kwa Maktaba Kuu ya Zanzibar ili kutowa huduma kwa Wanafunzi na Wananchi wanaopata huduma katika Maktaba hiyo Maisara.
MKURUGENZI wa Huduma ya Maktaba Kuu Zanzibar Sichana Haji Fuom, akitowa shukrani kwa Familiya hiyo kwa Msaada wao wa Mashine ya Fotokopi kwa ajili ya matumizi ya Maktaba Kuu Zanzibar.
MWAKILISHI wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akisisitiza jambo akiwa na Mkurugenzi wa Maktaba Kuu Zanzibar Sichansa Haji baada ya kukabidhi Msaada wa Mashine ya Fotokopi iliotolewa na Familiya ya Sheraly, kulia Abass Mahmoud , wakiwa chumba cha Internet katika jengo la Maktaba Maisara.
No comments:
Post a Comment