Habari za Punde

BODI YAZIPIGA KAMBA HUDUMA, MUEMBE MAKUMBI DISPENSARY

Na Fatma Kassim, Maelezo

BODI ya Ushauri wa Hospitali Binafsi imezifungia hospitali mbili za binafsi ziliopo katika maeneo ya Muembemakumbi baada ya hospitali hizo kutofanyakazi zake kama inavyotakiwa.


Hospitali hizo ni pamoja na Muembemakumbi Dispensary na kliniki iiitwayo Huduma ambazo zimepigwa marufuku kutoa huduma kutokana matatizo ya mbali mbali ikiwemo tatizo la wafanyakazi pamoja na kutoridhisha usafi wa hospitali hizo.

Msaidizi Mrajis wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi Dk. Shaaban Seif Mohammed amesema sababu nyengine ya kufungiwa Muembe makumbi Dispensary ni kutokuwa na wafanyakazi wenye sifa za kutoa huduma za afya.

Alisema kutokauwa na wafanyakazi wenye sifa za kutoa huduma za afya kwa binadamu kunaweza kukahatarisha maisha ya wananchi wanaofika kupatiwa huduma katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa kasoro nyengine ni uchafu wa taka taka za mabomba ya sindano ambayo yametumika kwa muda mrefu bila kutupwa na kusabaisha uchafu mkubwa katika hospitali hiyo.

Adha alifahamisha kuwa kwa upande wa hospitali ya Huduma haina wafanyakazi wa kutoa huduma za kihospitali na wamewakuta wafanyakazi wa karibu wa mmliki wa hospitali hiyo wakiwa wanatumiwa kuuza dawa.

Alitoa tahadhari kwa wananchi wanaotumia hospitali hizo kuwa wasizitumie kwa sasa kwani zinaweza kuhatarisha afya zao kwa kukiuka kanuni za afya.

Alifahamisha kuwa Bodi yake itahakikisha inazipitia mara kwa mara hospitali hizo ili kuhakikisha marufuku hiyo wanaitekeleza na wasiweze kutoa huduma kinyemela hadi hapo watakaporekebisha matatizo yaliyopo.


Aliwataka wamiliki wa hospitali hizo kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyomo katika hospitali zao ili ziweze kutoa huduma kwa umakini kwa wananchi wanaohitaji huduma hizo.

Aisema kuwa wamiliki wengi wa hospitali binafsi huwa wanajali kupata fedha tu na sio kutoa huduma zinavyotakiwa jambo ambalo ni kinyume na utoaji wa huduma za kiafya.

Bodi hiyo imeweza kuzifungia hospitali mbali za Unguja na baada ya kurekebisha imezifungulia na hospitali zinatoa huduma kwa mujibu washeria zilizowekwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.