Mamia ya Wananchi,Viongozi wa Serikali, siasa,Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameshiri katika arubaini ya kumuombea dua aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Baraza la wawakilishi Marehemu Maalim Mussa Silima.
Arubaini hiyo ya Marehemu Maalim Mussa Silima imefanyika Kijijini kwao Kiboje Wilaya ya Kati na Kuhudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Marehemu Maalim Mussa alifariki Dunia akitanguliwa na Mkewe Marehemu Bi Mwanakheir Talib baada ya kupata ajali ya gari wakitokea Mjini Dar es salaam kuelekea Dodoma.
Bibi Mwanakheir amefariki Dunia muda mfupi tu baada ya ajali hiyo wakati Muwewe alifariki baada ya Siku mbili.
Akitoa mkono wa pole Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameitaka familia ya Maalim Mussa kuwa na Subira katika kipindi hichi huku wakikumbuka kwamba kila Nafsi itaonja mauti.
Mapema asubuhi Balozi Seif akiwa pia Mbunge wa Jimbo la Kitope amewatembelea Wanafunzi 26 wa Darasa la Saba na la 11 wa Skuli ya Kilombero walioweka Kambi kwa ajili ya kujiandaa na Mitihani yao inayotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Akikabidhi vyakula kwa wanakambi hao ili kuendelea vyema na masomo yao ya ziada katika njia ya utulivu Balozi Seif amewapongeza walimu na wazazi kwa uwamuzi huo utakaowawezesha vijana hao kukabiliana vizuri na Mitihani yao.
Amesema Sera ya Serikali ni kuona kila Skuli ina Darasa la 12, hivyo ameiagiza Kamati ya Skuli hiyo kukabiliana na Changa Moto hiyo kwa lengo la kwenda Sambamba na Sera hiyo.
Wakati huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amefanya ziara ya ghafla katika Kisima cha Maji Safi kiliopo Ghana Bumbwisudi.
Balozi Seif amewaagiza Wahandisi wa Mamlaka ya Maji {ZAWA} kuhakikisha wanatoa taarifa mara moja kwa masheha wakati wanapofanya marekebisho katika Visima hivyo.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa Shutuma zinazotolewa na Wananchi dhidi yao ambazo amekuwa akilalamikiwa na kuripotiwa kila wakati.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment