
Mtaalamu wa Kilimo cha mbogamboga Bi Salma Marshed akimuonesha shamba darasa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi wakati alipotembelea shamba la mbogamboga la wana ushirika wa mwendo wa Jongoo liliopo kijiji cha Kazole kilichopo ndani ya jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope akimkabidhi mipira ya maji Katibu wa ushirika wa kilimo cha mbogamboga kiitwacho mwendo wa jongoo Bw, Moh,d Amour Kombo mara baada ya kutembelea shamba la wana ushirika hao, na kuwataka waitumie mipira hiyo kwa kilimo cha umwagiliaji.

Mbunge wa jimbo la Kitope na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Mhe Vuai Ali Vuai wakisaini hati za makabidhiano ya jengo la ofisi ya Mbunge wa Kitope wakati wa sherehe ya makabidhiano ya ofisi hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Mhe Vuai Ali Vuai akimkabidhi rasmi jengo la ofisi ya Mbunge wa Kitope Mhe Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa jimbo hilo. Jengo hili limegharimu Sh,milioni 40 zimetolewa na ofisi ya bunge na ujenzi umesimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B,

Jengo la ofisi ya mbunge wa jimbo la Kitope.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Ujenzi wa Afisi za Wabunge ndani ya Majimbo ni uamuzi sahihi wa Bunge La Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha huduma za Wananchi zinapatikana kwa haraka muda wote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa Afisi ya Jimbo hilo baada ya kukamilika Ujenzi wake.
Hati za Makabidhiano ya Afisi hiyo ya Mbunge wa Kitope imetiwa saini kati ya mbunge huyo Balozi Seif na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Nd. Vuai Ali Vuai ambapo ujenzi wa Afisi za Wabunge unasimamiwa na Afisi za Wakuu wa Wilaya.
Akikabidhi hati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakaskazini B Nd. Vuai Ali Vuai amesema ujenzi huo unafuatia azimio la bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa kujenga Afisi za Wabunge Majimboni.
Akipokea Afisi hiyo mbunge wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia wananchi hao kwamba yeye na mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Makame Mshimba wataendelea kushirikiana na Wananchi hao ili Maendeleo ya haraka ndani ya Jimbo hilo yafikiwe.
Wakati huo huo Balozi Seif Ali Iddi ameutembelea ushirika wa mwendo wa jongoo wa Kazole ambao unajishughulisha na ukulima wa mboga mboga.
Akiunga mkono juhudi za wanaushirika hao Balozi Seif Amekabidhi ndondo kwa kuendeleza ujenzi wa Afisi ya Tawi la CCM la Kijiji hicho pamoja na mpira wa Maji na vifaa vyake na kuahidi kutoa makalbi ya kisima ili kuwaondoshea shida ya upatikanaji wa maji katika mradi wao wa kilimo.
Balozi Seif pia amekabidhi msaada wa Matofali, Saruji, mchanga na fedha za fundi kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Tawi la CCM La Kichungwani na kushauri ni vyema Tawi hilo likaanza kutoa huduma mwaka ujao.
Vifaa na msaada huo kwa Kikundi cha Ushirika cha Uwendo wa Jongoo na Afisi za CCM vimegharimu Shilingi Milioni Moja Nukta Moja.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Huyu mzee kwa kweli anajitahidi na amekua mfano wa kuigwa.kwanini wabunge wengine wasiige mfano huu? mathalan,suala la kusaidia kilimo angalau cha mboga mgoga.hivi mpaka lini visiwa hivi vitaendelea kutegemea mboga mboga kutoka bara? wabunge wengine kwa kweli wanatuangusha! hawana ofisi ktk majimbo yao wala hawapiti, wengine wana mawazo kua wataombwa pesa. wakumbuke kua sio wote wenye tabia hizo.wengine tuna mchango mzuri wa mawazo yatayosaidia kuboresha maendeleo jimboni na kumfanya mbunge mwenyewe azidi kung'ara.wangetoa angalau namba za simu kwa wale wenye michango mizuri.mfano jimboni kwangu niliombwa msaada wa kuingiza umeme,nilisikitika kugundua kua nimechangia mara 3 zaidi ya mbunge anaenizidi kwa kipato.big up balozi seif,hapo umepatia.wasiwasi ni tu juu ya gharama halisi za huo ujenzi wenyewe...naona kama 40m.ni nyingi mno kulingana na ofisi yenyewe?
ReplyDeleteNafikiri nikweli mh huyu anajitahidi sana na anastahili pongezi kwa juhudi anzozifafanya jimboni kwake lakini mimi pia nimeshangazwa na gharama za ujenzi kulinganisha na jengo lenyewe hapa nahisi pana harufu ya u.......... any way jamaa anajitahidi ila kwa upande wa namba za simu wenzetu india nje ya nyumba ya mbunge utakuta kibao kimeandikwa nambari ya simu ya mbunge hivyo nirahisi kumpata kwa simu na inawasaidia hata wasiopajua anakokaa mbunge kupajua.
ReplyDeleteAhsante Kakhtan, kwa kutufungua macho! kumbe kama wangechukua hiyo idea ya India wasingekosa cha kusema pale bungeni tunge 'watextia' vitu vya maana tu badala ya kwenda kufanya vituko.hawa jamaa kwa kweli wanatuchosha.Angalia kama kule Pemba utakuta skuli,darasa la watoto 40 form 4 wamepasi 3.ukiuliza utaambiwa upungufu wa waalim na vitabu vya kufundishia,hivi kweli mbunge anashindwa kushirikiana na wadau(tupo)akatafuta walimu wa masomo ambao wanakosekana? mfano hivi ina gharimu kiasi gani kumsafirisha na kumlipa mwl.wa Math kwa muda wa miezi 2 kucover topics za form4, ikiwa mwl.mwenye degree mwezi mzima analipwa laki 2? au vitabu? huwezi kuamini lkn kuna shule hata dictionary hazina kazi kulaumu serikali tuu! wakati umefika tisiangalia sura wala vyama vyetu... maendeleo kwanza! Kakhtan, wahamasisheni vijana ndugu, tubadilishane mawazo kupitia hii blog..tutafika tuu,"united we stand,devided we fall"
ReplyDeletehili jengo hata mtoto mdogo hawezi kukubali kama limeharimu milion 40
ReplyDelete