Jumuiya ya Watanzania iliandaa Dua Maalum katika Chuo Kikuu IIUM kuwarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya "MV Spice Islanders"
Watanzania walijitokeza kwa wingi toka majimbo kadhaa nchini Malaysia na kushiriki katika maombi hayo maalum yaliyofanyika baada ya Sala ya Ijumaa tarehe 16 Septemba 2011. Ubalozi wa Tanzania uliwakilishwa na Kaimu Balozi Bw. Simba Yahya, ambaye kwa niaba ya Ubalozi, alifikisha salamu za pole kwa wanajumuia walioathirika moja kwa moja, na kwa watanzania kwa ujumla kwa kupoteleza idadi kubwa ya maisha ya Watanzania katika ajili hiyo.
Mungu Ibariki Tanzania. AMEEN.
No comments:
Post a Comment