Habari za Punde

SUALA LA MDAU - KALENDA ILIYOPO YA SAUDIA AU ZENJ?

Assalaamu Alaykum

Bwana Maulid, mimi ni mmoja ya wadau wako wa blog yako adhimu lakini nina suali juu ya hiyo Kalenda ya kiislam je wewe binafsi unafuata wapi? SAUDIA? au unafuata ZNZ? kwani Kalenda yako inaonesha leo 26 sep 2011 ni sawa na 28 shawal sawa na SAUDIA, wakati mwezi ZNZ ulionekana 30st aug ikiwa na maana tumepishana siku 1 tu tofauti unavyoonesha wewe kwenye blog yako siku 2 .Kwa uwelewa wangu leo ni 27shawal Zanzibar. EID ILIKUWA 31ST AUG.


Sasa naomba utuekee wazi ni wapi kalenda yako inafuata ZNZ au SAUDIA ili tujue kwani kuna wanaofuata Saudia na wengine Znz.

Natanguliza samahani zangu juu ya hilo.

Wako mdau

Tunakushukuru sana Mdau kwa kututembelea na pia kutuuliza suala ambalo tumeona kwa faida ya wengine tuliweke kwenye Blog ili waweze kufahamu na pia kuchangia.


Tulipoweka Kalenda hii yenye tarehe za mwaka wa kikristo na  kiislamu tuliiweka kwa lengo la hasa Waislamu wajue tarehe za kiislamu ambazo wengi huzifuatilia karibu ima katika Ramadhaan na Hija ama kwa siku nyengine huwa hawana habari nazo. Hivyo Madhumuni makuu ni kuwajuulisha wanaotembelea tarehe za kiislamu.


Pili hizi Kalenda zipo katika template codes ambazo sisi ni kucopy na kupaste katika Blog hatuna uwezo wa kuzirekebisha au kubadilisha.


Tatu si suala la ufuasi kwamba tunafuata wapi bali ni suala la kupeana taarifa tu ya tarehe. Kama kukiwa na haja ya kuwepo tarehe zote ni kwenu Wadau mtujuulishe nasi tufanyie kazi


Shukran


Jikumbuke Blog





1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.