Habari za Punde

DK SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHINA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa madaktari kutoka katika jimbo la Jiangsu nchini China,ujumbe huo ulifika ikulu Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais,ni katika kuimarisha sekta ya Afya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa Madaktari kutoka China Naibu Mkuu Idara ya Afya katika jimbo la Jiangsu,Zhou Zhengxing,ikulu mjini Zanzibar,jana ujumbe huo umekuja katika kuimarisha sekta ya Afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na ujumbe wa madaktari kutoka jimbo la jiangsu,nchini China ukiongozwa na Naibu Mkuu Idara ya Afya katika jimbo hilo,Zhou Zhengxing,(wa pili kushoto),pia Balozi mdogo wa China anyeishi Zanzibar,Chen Qiman, aliongoza ujumbe huo,Ikulu Mjini Zanzibar jana

Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

1 comment:

  1. Kama madaktari hao, watakua nchini kikazi basi wapewe usimamizi wa karibu.Isije ikawa wamemaliza mafunzo huko kwao wanakuja kwetu kufanya mazoezi ya vitendo(practical)..Tukumbuke kusomesha madaktari ni gharama hivyo mtu kukupa daktari mwenye ujuzi na uzoefu sio rahisi..tuwe macho!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.