Habari za Punde

BARAZA LA IDD PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akitowa hutuba yake wakati wa sherehe za kitaifa za Baraza la EId Al Hajj.zilizofanyika jana katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi Wete Pemba
>Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akimpa mkono wa Eid mkewe Mama Mwamamwema Shein,wakati wa kusherehekea sikukuu ya Eid Al Hajj,baada ya kumalizika baraza la Eid Hajj,huko Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akiwapa mkono wa Eid Al Hajj,akima mama wakati wa sherehe za Baraza la Eid Al Hajj,lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Mkoa wa kaskazini Pemba.


Baadhi ya akinamama wakiwa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba,katika mkutano wa Baraza la Eid Al Hajj,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlHaj Dk Ali Mohamed Shein,alipohutubia Baraza hilo,lililohudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa,Mawaziri wa Serikali ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akipokea slamu ya heshma ya paredi la kikosi cha polisi (FFU),wakati wa sherehe za Baraza la Eid Al Hajj,zilizofanyika jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba

Askari wa kikisi cha Polisi cha (FFU) Pemba,wakitoa salamu ya heshma kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi AlHaj Dk Ali Mohamed Shein,wakati alipowasili katika viwanja vya Baraza la wawakilishi Wete Pemba,katika sherhe za baraza la EId Al Hajj,lililofanyika jana katika ukumbi wa Baraza hilo

Picha na Ramadhan Othman, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.