Habari za Punde

KAMPUNI YA USAFIRI WA BAHARI SEAGULL YADHAMINI LIGI KUU YA ZANZIBAR NA KUITWA SEAGULL.

 KOCHA Mkuu wa timu ya Mafunzo Omar Kigani akiwapa maelekezo wachezaji wake wakati wa mapumziko
 KOCHA Mkuu wa timu ya Mundu Hemeid Moroco akiwapa maelekezo wachezaji wake jinsi ya kupata ushindi katika mchezo wao wa ufunguzi na timu ya Mafunzo uliofanyika uwanja wa Mao.
 KOCHA Msaidizi wa timu ya Mafunzo, Mohammed Kachumbari akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.  
 WAPENZI wa timu ya Mundu wakifuatilia mchezo wa timu yao na wapinzani wao timu ya Mafunzo uliofanyika uwanja wa Mao.  

 MCHEZAJI wa timu ya Mundu, Suleiman Mohammed (kushoto) na beki wa timu ya Mafunzo, Kheri Kondo wakiwania mpira katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Seagull iliofanyika uwanja wa Mao.  
 MSHAMBULIAJI wa timu ya Mafunzo, Mohammed Abrahaman akimpita beki wa timu ya Mundu Ame Juma.(kushoto)  

 HIVI ndivyo ilivyokuwa hekaheka za mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Seagull katika uwanja wa Mao kati ya timu ya Mundu na Mafunzo.
 MCHEZAJI wa timu ya Mundu Keneth Faustin  akiwapita mabeki wa timu ya Mafunzo katika mchezo wa ligi kuu ya Seagull uliofanyika uwanja wa Mao. 
 MSHAMBULIAJI wa timu ya Mundu kushoto na beki wa timu ya Mafunzo Jaku Juma wakiwania mpira katika mchezo wa ligi Kuu ya Seagull uliofanyika uwanja wa Mao timu hizo zimetoka sare 0--0   
Beki wa timu ya Mundu, Kombo Khamis (kushoto) akiokoa mpira katika mchezo wa Ligi Kuu ya Seagull, huku mchezaji wa timu ya Mafunzo kulia Sadik Habib akijaribu kumzuia. Timu hizo zimetoka sare ya 0-0.   
MAKOCHA wa timu ya Mundu  Hemed Morocco (kushoto) na Omar Kigani  wa Mafunzo, (kulia) wakipongezana baada timu zao kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya Seagall Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao.

2 comments:

  1. Mapara kuwa muangalifu, wote wapo kulia sasa yupi yupo kushoto hapo.
    Makame Hj KL

    ReplyDelete
  2. Wakati mwengine uchofu Bro, Tumerekebisha

    Shukran kwa kututanabahisha

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.