TAMASHA la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka hapa Zanzibar, liko katika hatari ya kuhama kwenda nje ya nchi, endapo halitapata nguvu za ziada kwa kuungwa mkono na taasisi na wafanyabiashara wa ndani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya 'Busara Promotions' Yussuf Mahmoud, wakati wa mkutano wa viongozi wa taasisi za kitalii pamoja na wafanyabiashara, uliofanyika juzi katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini.
"Inauma, lakini yanibidi niseme kwamba, ikiwa hatuwezi kupata msaada zaidi kutoka serikali za mitaa na wafanyabiashara, tamasha la mwaka 2012, huenda likawa la mwisho kufanywa na Sauti za Busara hapa Zanzibar, kwani tutalazimika kulihamishia Dar es Salaam au kwengineko",alifafanua Mkurugenzi huyo.
Alieleza kuwa, matamasha mengi duniani, yakiwemo ya Afrika, hupata mchango kutoka manispaa, serikali za mitaa na serikali kuu, lakini bado Sauti za Busara halijapata mchango kutoka serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
Alifahamisha kuwa, badala ya kupokea michango kutoka Baraza la Sanaa Zanzibar (BASAZA) au serikali za mitaa, lakini kinyume chake, Busara inalipa dola elfu kadhaa kila mwaka kwa baraza hilo kwa ajli ya leseni na vibali vya wasanii.
Aidha alitaja malipo mengine yanayotozwa, ni kulipia Bodi ya Sensa, Wizara ya Habari kwa ajili ya vibali vya waandishi, manispaa kwa kuweka posta za matangazo mitaani, Uhamiani (viza za wasanii), pamoja na malipo ya kumbi za burudani kama Ngome Kongwe.
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa taasisi yake iko katika wakati mgumu sana wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato, ili kulifanya tamasha hilo liwe endelevu.
Aliweka wazi kuwa, ofisi za kibalozi jijini Dar es Salaam, zimekuwa zikiwauliza sababu ya kuendelea kuziomba pesa wakati serikali na wafanyabiashara wanaingiza mapato mengi katika kipindi cha tamasha kutoka kwa wageni.
"Wachangiaji ambao wanalichangia tamasha wametuambia kuwa, njia bora ni PPP (Public Private Partnership), yaani ushirikishwaji wa sekta za umma na binafsi", alisema.
Wengine wetu tunatilia shaka sababu za kweli zitakazopelekea tamasha la Busara kufunga virago mbali na kuhusu kosefu wa michango kutoka kwa serikali na wafanya biashara. Kwa mtazamo wangu, ilikuwa ni vyema Mkurugenzi wa Busara Promotions akaeleza changamoto zinazohusiana na tetesi kuwa wadhamini wamevunjika moyo kwa kuona kuwa tamasha hilo halina matumaini ya uendelevu kwa sababu zizisohusu gharama za uendeshaji na ndiyo kwa maana wameanza kuwatupa mkono. Kati ya sababu hizo ni pamoja na ukosefu wa kuwa na ushirikishwaji wa kutosha wa vikundi vya Zanzibar na baadili yake kupewa kupaumbele wasanii kutoka nje kwa gharama kubwa jambo amablo ni la kujifakharisha bila ya kuwa na uwezo wa kifedha. Pili ni kuendelea kufanyika kwa programu zisizo na ubunifu ambazo kwa wanaolifahamu tamasha la ZIFF ni 'copy paste' kuanzia parade hadi mwisho. Tatu, ni kuendelea kuliweka tamasha hilo katika mazingira ya kitalii zaidi na mara nyengine kvuka mipaka na kuwa sehemu ya kuuza ulevi kwa wingi na hivyo kupelekea kuvunjika kwa maadili na kuwakera wananchi. Nne, ni kukuso mwelekeo wa kizalendo kwa taasisi hoyo kutukuwa na mpango maalumu wa kuwa na viongozi watendaji kutoka Zanzibar. Hadi sasa, hakuna Mzanzibari yoyote katika safu nzima ya uongozi wa taasisi hiyo ambayo inaonesha kuwa hawathamini uwezo wa waZanzibari katika kuendesha miradi na taasisi za sanaa kwa ufanisi. Mbali na sababu nyengine nyingi ni mihimu pia kutafakari kuwa hata ikiwa tamasha hilo litahamia popote pale basi Zanzibar haitoshindwa kuwa na tukio jengine kama hilo ambalo pengine huenda likawa na faida zaidi kiutamaduni na kiuchumi kwa Zanzibar na wasanii wake
ReplyDeleteMaelezo mengi, ukweli kidogo! kwa ufupi wa Zenj hatuna utamaduni wa kuchalia mambo! haiwi msikitini watu wanatoa 'mia' tuu! misikiti yote inajengwa na Waarabu! tazama msiba wa Spice Islander misaada karibu yote ilitoka nje ya ZNZ. Vikundi vyote vya taarab vimehamia bara. Hiyo kua sisi hatupewi nafasi ishakua wimbo wa taifa, tushachoka kusikia!..mambo mambo ukitaja pombe ndio ohooooo! lkn ukiona au ukisikia yanayofanyika mitaani Zenj, utatapika!
ReplyDelete