Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku mara moja ambapo kuanzia sasa hakuna taasisi, kampuni au wakala yeyote atakayeruhusiwa kusafarisha watu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi.
Kauli hiyo nzito ya Serikali imetolewa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema amri hiyo ni ya Serikali na atakayekwenda kinyume na amri hiyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Mhe Haroun amesema Serikali imelazimika kuchukua maamuzi hayo kutokana hivi sasa kuwepo malalamiko mengi ya wananchi kuonewa na kunyimwa haki zao huku Afisi za ubalozi za Tanzania zilizopo nje zimetaka uhakika wa mikataba kabla ya mwananchi kwenda kufanya kazi nje.
Pamekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi hasa vijana kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kupelekwa nje lakini wengi wamekuwa wakitapeliwa huku mawaklaa wakikimbia na wengine wakishindwa kurejesha fedha .
Wakaazi wengi wa Zanzibar hupendelea nchi za Dubai,Oman na Qatar kwa ajili ya ajira.
Sambamba na hilo, lakini Waziri huyo alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatuma ujumbe wake kufuatilia hali hiyo katika nchi husika.
Sambamba na hilo, lakini Waziri huyo alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatuma ujumbe wake kufuatilia hali hiyo katika nchi husika.
Sambamba na uamuzi huo, Waziri Haroun, alisema kumejitokeza baadhi ya watu ambao huwafungisha mikataba ya safari watu wanaotaka kazi, ambao kwa sasa fedha hizo zimesharejeshwa kwa wahusika.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Haroun ameiomba Idara ya Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kusimamia suala hilo na kuzuia watu wa aina hiyo hadi hapo Serikali itakapolifuatia kwa undani zaidi.
No comments:
Post a Comment