Habari za Punde

TASINI YAVUNA KARAFUU

Na Abdi Suleiman, Pemba

LIGI daraja la tatu Wilaya ya Mkoani, imeendelea kurindima katika kiwanja cha Mkanyageni, kwa timu ya Tasini kuichapa Karafuu mabao 3-0.

Suleiman Nassor ndiye aliyeanza kuzifumania nyavu za timu ya Karafuu katika dakika ya pili, huku Khamis Salum akipachika bao la pili katika dakika ya 27, na matokeo hayo kudumu hadi wakati wa mapumziko.

Licha ya Karafuu kupania kusawazisha mabao hayo, lakini ilijikuta ikichomekwa bao la tatu mnamo dakika ya 78 lililofungwa na Khamis Abdalla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.