Habari za Punde

UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA SINGAPORE WAWASILI ZANZIBAR

 Maelezo Zanzibar

Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Singapore ukiongozwa na Waziri wa Biashara na Viwanda umewasili Zanzibar leo asubuhi kwa ziara ya siku moja.

Kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ujumbe huo ulipokelewa na Naibu Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar Thuweiba Kisaasi , Mwenyekiti wa Jumuiya ya 


Wafanyabiashara Viwanda na Wakulima Zanzibar Mbarouk Omar pamoja na maofisa mbali mbali katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar.

Kwa mujibu wa Ratiba iliotolewa na Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar , Ujumbe huo mchana huu utakuwa na mazungumzo na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd hukoOfisini kwake Vuga.

Usiku Kwenye Hoteli ya Serena iliopo Mjini Zanzibar Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore ataelezea juu ya hali ya Biashara nchini mwao na baadae kutatolewa maelezo juu ya nafasi za Vitega Uchumi viliopo Hapa Zanzibar.

Aidha Kamisheni ya Utalii Zanzibar nayo itapata nafasi kuelezea juu ya nafasi ziliopo Zanzibar katika mambo ya utalii na baadae kuwa na Chakula cha Usiku pamoja na kuwa na mazungumzo na Wafanya biashara wa Zanzibar na Wanasiasa.

Ujumbe huo Wawafanyabiashara kutoka Singapore ukiongozwa naWaziri wa Biashara na Viwanda unatarajiwa kuondoka Zanzibar hapo kesho asubuhi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.