Habari za Punde

'MNAOMALIZA VYUO VIKUU MJIAJIRI'

Na Madina Issa

WANAFUNZI wanaojiunga vyuo vikuu mbali mbali nchini wametakiwa kujitengezea mazingira mazuri ya kujitafutia ajira wanapomaliza masomo.

Ushauri huo umetolewa na mtaalam wa Computer, Profesa Othman Naomba alipokuwa akiwasilisha mada juu ya fursa ya ajira kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo hicho.


Aliwaambia wanafunzi wa Chuo hicho katika semina maalum iliyoambatana na maonesho ya kazi mbali mbali za SUZA iliofanyika ukumbi wa Chuo hicho Vuga.

Alisema kila mwanafunzi anayesoma chuoni hatua ya mwanzo huwa anafikiria ajira hivyo ni vyema pia afikirie kufanya vizuri ili aweze kujiajiri mwenyewe.

"Hivi sasa wamejitokeza baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali kutokuwa na malengo ya kujitafutia ajira wenyewe na kutegemea serikali hili si jambo zuri kwa wasomi kama nyinyi," alisema Profesa Othman.

Profesa Othnan alisema fursa za kujiajiri zipo nyingi kwa wasomi lakini uwezekano wa kuajiriwa ni mdogo kutokana na kwa matatizo ya mawasiliano kati ya waajiri na wanaotaka ajira.

Hata hivyo, alisema nafasi za ajira zipo lakini zinahitaji watu wenye uwezo na wawe wabunifu sambamba na kuweza kutumia Computer kikamilifu.

Aidha amefahamisha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu wana nafasi nzuri ya kutumia elimu yao kwa kujiajiri na kutosubiri ajira kutoka Serikalini na baada yake watumie elimu yao kwa kuweza kujiajiri wenyewe.

"Msomi yoyote anayejiamini na mwenye uwezo wa kutosha hanabudi kujitafutia ajira mwenyewe hata kwa kufungua skuli pia sio mbaya,"alisema Profesa Othman.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiswahili na lugha za Kigeni (TAKILUKI), Mmanga Mjengo Mjawiri amewataka wanafunzi wa chuo cha SUZA kujifunza elimu ya stadi za maisha ili waweze kuwa na nafasi ya kujiajiri na kuajiriwa.

"Mwanafunzi yoyote atakayeweza kujifunza elimu ya stadi za kimaisha ataweza kujipatia ajira mwenyewe binafsi ama kuajiriwa," alisisitiza Mkurugenzi huyo.

2 comments:

  1. Ni sawa alivyosema huyu profesa. Lakini mitaala ya chuo ndio inayowezesha wanafunzi kuwa na uwezo wa kujiajiri. Mitaala yetu ya zamani ilikuwa haimuwezeshi mwanafunzi kujiajiri lakini kama itafanyiwa marekebisho basi ni kweli watu wanaweza kumaliza shule na kujiajiri.

    ReplyDelete
  2. Tupeni na nyezo za kujiariji yaani ukisoma unaomba mkopo than unasubiriwa uje uulipe ila hakuna nyezo za kujiajiri wao wa juu wanajipandikizia mimali na sisi walala hoi ndio tunazidi kuumia kila kukicha

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.