Habari za Punde

WAZAZI WAHIMIZWA KUPELEKA WATOTO HOSPITALI

Na Khamisuu Abdallah

KATIBU Mkuu Jumuiya ya Zanzibar Outreach Program (ZOP) inayosaidia jamii kwa matibabu ya macho, koo, pua, presha, Naufal Kassim Muhamed amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu na waoto wao na
wanapowabaini na matatizo ya kiafya kuwapeleka hospitali kwa matibabu.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa kuwaaga wagonjwa waliopatiwa matibabu ya upasuaji wa masikio na jumuiya hiyo katika hospitali ya Mnazimmoja.


Dk.Naufal alisema kila mzazi anapobaini matatizo kwa mtoto wake amuwahishe hospitali haraka kuchunguzwa afya yake ili aondokane na maradhi yanayomsumbua.

Alisema watoto wengi waliofanyiwa upasuaji huo walikuwa wana matatizo ya kutoboka kwa ngome za tundu ya sikio na kusababisha kutoka usaha mwingi masikioni hali iliyofanya hata kutosikia.

"Watoto wengi waliofanyiwa upasuaji wiki iliyopita, wamegundulika na matatizo ya kutoboka kwa ngome ya tundu za sikio ndio kilichofanya kutosikia vizuri", alifahamisha Dk.Naufal.

Mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji na jumuiya hiyo Omar Khamis kutoka Bagamoyo Mtambwe Pemba, na tokea apate upasuaji hali yake imeanza kustawi vizuri.

“Tokea nifanyiwe upasuaji huo nimekuwa nasikia vizuri kwani hapo mwanzo nilikuwa sisikii na kwa sasa nashukuru,"alisema Omar.

Hata hivyo, madaktari hao wameombwa kuzitembelea skuli mbali mbali, ikihofiwa kwamba wapo vijana wengi wenye matatizo kama hayo wakihitaji kufanyiwa upasuaji na huduma nyengine za kiafya.

Wagonjwa 27 wamefanyiwa upasuaji na jumuiya hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.