Habari za Punde

WAZIRI MIUNDO MBINU AKEMEA UZEMBE BARABARANI

Na Fatma Mzee Maelezo Zanzibar


Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masud amema kuwa serikali imechoshwa na kuona kesi nyingi za usalama barabarani huachwa na kutupiliwa mbali kwa kile kinacho daiwa huwa hazina ushahidi wa kutosha .

Hivyo aliwataka askari wa usalama barabarni wabadilike ili kuona kesi za ajali za barabarani zinachukuliwa hatua madhubuti za kisheria ili aliye fanya kosa ahukumiwa kwa mujibu wa sheri.

Alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wamechoshwa kuona uvunjwaji wa sheria za barabarni na vifo vinavyo tokana na ajali hizo.


Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar Dk Shein katika uzinduzi wa muongo wa Taifa wa usalama barabarani huko kati Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar .

Aidha alisema kuwa wizara yake ya mawasiliano inajipanga upya ili kuona ajali za barabarani zinapunguwa kwa kiasi kikubwa.

Mapema waziri Hamad Masud alikiri kwamba zipo gari ambazo hazina viwango vya kutembea barabarani na kuzidi kusababisha idadi kubwa ya ajali barabarani pamoja na kuharibu mazingira kwa kutoa moshi kupita kiasi barabarani.

Alisema atahakikisha gari kama hizo hazitopata leseni za kutembea barabarani na aliongeza kuwa utaratibu wa utoaji wa leseni utarekebishwa na kuhakikisha kuwa sehemu moja tu ndio itakayokuwa inatowa leseni kwa vyombo vya moto.

Pia alizungumzia Magari makubwa na mdogo yanayo tembea usiku yakiwa na taa moja au hazina taa kabisa husababisha idadi kubwa ya ajali hizo .

Tatizo la ubovu wa barabara na alama za barabarani pia huchangia ajali ,waziri ameahidi kuboresha kitengo kilichokuwepo cha utunzaji wa barabara.

1 comment:

  1. Tunaomba pia, muingize somo la 'driving tolarance' katika mitaala ya udereva. Z'bar yenye watu wachache na idadi ndogo ya magari, tunashindwa na D'slam, dereva anasimamisha gari na kumuomba mtembea kwa miguu avuke wakati znz hakuna kitu cha namna hiyo lakini zaidi, utaskia"wacha kucheza barabarani!"

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.