Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakisikiliza mada kwenye semina waliyoandaliwa kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla wakati akitoa mada ya historia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi hapo MbweniPicha ya pamoja kati ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na wajumbe waliohudhuria semina kuhusu mtangamano wa jumuiya ya afrika mashariki iliyofanyika hapo Mbweni.
Kulia ya balozi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Stergomena Tax, Naibu Waziri Dr. Abdulla Juma Abdulla na Waziri wa Ustawi wa Jamii Zanzibar Mh,.Zainab Mohammed.
Kushotoni mwa Balozi ni Spika wa blw Mh. Pandu Ameir Kificho, waziri wa nchi ofisi ya rais na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dr. Mwinyihaji Makame na mwakilishi wa jimbo la Mfenesini Mh. Ali Abdulla Ali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua semina kuhusu mtangamano wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa juu wa mikutano wa jengo la baraza la wawakilishi liliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Bidha zinazozalishwa ndani ya Afrika Mashariki zinaweza kupata soko la uhakika iwapo wazalishaji wa bidhaa hizo watazitengeneza katika kiwango kilicho bora Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiifungua Semina kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema cha msingi kusisitizwa Wananchi ni kuwa na Ujasiri wa kutumia fursa za Umoja wa Forodha na Soko la pamoja ili kujiletea Maendeleo.
Balozi Seif alisema Wananchi walio wengi bado wana uelewa mdogo kuhusu masuala ya Mtangamano wa Afrika Mashariki hali ambayo inawatia hofu katika hatma yao ya baadaye.
“ Wananchi watatuuliza maswali mengi na tutakuwa na wajibu wa kuwajibu na kuwafahamisha mpaka waelewe kwa lengo la kuzijua haki zao za Jumuiya ya Afrika Mashariki ”. Alifafanua Balozo Seif.
Alisisitiza kwamba uelewa mkubwa wa Mtangamano huo wa Afrika Mashariki ni muhimu katika kubuni mbinu za kukabilianan na ushindani ili kuweka mazingira bora ya kuongeza tija katika uzalishaji na utoaji huduma.
Balozi Seif alieleza matumaini yake kwa Zanzibar kujenga shauku kubwa ya kushiriki kikamilifu katika Mtangamano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya Afrika Mashariki kwa kuandaa Semina hii ambayo itasaidia Wawakilishi kuwajengea uwezo wa kuwahamasisha Wananchi katika kutumia fursa zilizopo za Biashara, Uwekezaji na Ajira ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akitoa Mada ya Historia ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrka Mashariki Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dr.Abdulla Juma Abdulla alisema ushirikiano wa Jamii ya Watu wa Kanda ya Afrika Mashariki upo kwa karne kadhaa zilizopita..Dr. Abdulla alisema kilichovuruga ushirikiano huo ambao ulihusisha Damu na Biashara ulivurugwa na Watawala wa Kikoloni walioingiza ubaguzi na kusababisha matabaka Miongoni mwa Jamii hizo.
Wakichangia mada mbali mbali zilizowasilishwa katika Semina hiyo Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameiomba Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuzingatia maslahi ya Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Wamesema suala la msuko suko wa Sarafu lililoikumba Dunia kipindi kilichopita limeathiri pia Uchumi wa Zanzibar na kushindwa kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa ambao umepanda kwa kiasi kikubwa.
Wameshauri kuwepo kwa Timu ya pamoja ya Wataalamu wa kilimo wa Nchi zote Wanachama wa Kanda ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuwa na sauti moja katika Sekta hiyo muhimu kwa Wananchi walio wengi wa kanda hii ya Afrika Mashariki.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zazbar
22/1/2012
Mimi, naamini z'bar haitapata maendeleo ya kweli mpaka pale tuu itapoamua kuipa umuhimu ELIMU ikwa ni pamoja na kutoruhusu watu wenye elimu ya chini ya degree moja kuchukua fomu za kugombea uwakilishi na ubunge.
ReplyDeleteJamani elimu muhimu!..ndio maana hata amri ya kwanza aliyoshushiwa Mtume ilikua 'ikra'(soma!)
na aya nyingine zikafata kama vile.."HAL-YASTAWI ALLADHINA..YAALAMUNA WA LLADHINA ..LA..YAALAMUN?
INNA MA YAKHSHA LLAHU MIN IBADIHI AL ULAMAA!..na nyingine nyingi.
Kinyume chake wenzetu ndio wanazitumia hizi aya.
Kwa kweli wasiosoma walipotufikisha panatosha! kwa mfano ktk semina kama hiyo..wameshika..nafasi ya Z'BA, nafasi ya Z'BAR ktk Afrika ya mashariki naamini wanakusudia nafasi za kisiasa.
Tumechoka kupewa nafasi za upendeleo, kwanza zinakua chache, lkn. pili wanawapa watu wasio elimu, na wakiwa na elimu hawana 'exposure'.. kw a hivyo sio 'threat' kwao na hawana msaada sana. kwetu
Hivi tunavyoongea, kuna safasi za kumwaga ktk jumuiya ya Afika masharika. na watu wanaomba kutoka kila kona na naamini vijana wenye sifa za namna hiyo za kielimu wapo lakini hawahamasishwi.