Habari za Punde

Wilaya ya Kilosa Yaibuka Kidedea Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango akikabidhi Tuzo na Cheti Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025, yaliyofika katika Mkoa wa Mbeya.          

MwenyeziMungu Mtukufu Muumba Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo tunakushkuru kwa uwezo na karama zako.

Aidha Shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutunuku Tunzo, Vyeti na  fedha  kwa washindi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 kitaifa.

Zoezi ambalo limefanywa kwa niaba yake na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Dkt Isidor Mpango katika viwanja vya Sokoine Mkoani Mbeya.

Sina la kusema zaidi ya kuwashkuru Mhe Adamu Kigoma Malima (RC Morogoro) na KU yake, wajuumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa, Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Kilosa DC, wakuu wa idara, maafisa Tarafa na watendaji wote wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri, kamati mbalimbali za Mwenge, Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025.

Pamoja  na wananchi wetu wapendwa wa wilaya ya Kilosa kwa  ushirikiano na kujituma kwao kwa kiwango cha juu kulikopelekea kupatikana kwa heshima hii na kuandika historia iliyotukuka kwetu.

Ushindi huu wa Mwenge wa Uhuru 2025 katika kanda yetu inayokusanya mikoa ya Tanga, Tabora, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Njombe na Morogoro yenyewe ni matokeo ya umoja, nidhamu, na moyo wa kizalendo uliotuunganisha kama familia moja ya wanakilosa.

Itakumbukwa kuwa Mwaka 2024 Wilaya ya Kilosa ilibuka mshindi wa Kwanza Kimkoa.

Asanteni wote kwa kuiletea wilaya yetu heshima hii kubwa na Mkoa wetu wa Morogoro kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.