Habari za Punde

MBUNGE MUYUNI AHIMIZA VIONGOZI KULIPATIA MAENDELEO JIMBO

Na Madina Issa

MBUGE wa Jimbo la Muyuni, Mahadhi Juma Maalim, amesema kuna kila sababu kwa viongozi kujipanga upya katika ngazi tofauti ili kuweza kushinda katika chaguzi mbalimbali zijazo.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya Jimbo la Muyuni juu ya kutathmini michango mbalimbali iliyotolewa kwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi wao.


Alisema endapo viongozi watakajipanga kwa kuwa na ushirikiano wataweza kuliletea maendeleo zaidi Jimbo lao.

Hivyo, amewataka viongozi hao wazidishe ushirikiano na viongozi wao wakuu kwa kuanzia ngazi ya Shina,Tawi,Wadi hadi Jimbo ili waweze kujiletea maendeleo ya pamoja.

“Kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wanawatupia lawama viongozi wao wakuu kwa kuwaona hawafanyi kazi ya chama hili sio jambo jema”alisema Mbunge Mahadhi.

Hata hivyo, aliwataka viongozi jimboni humo wakabiliane na changamoto zilizojitokeza na hivi sasa, wawe kitu kimoja kwa kuweza kunyanyua maendeleo zaidi ili kuyafikia malengo ya maendeleo yalifikiwa kwa
pamoja na viongozi katika Jimbo hilo.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Muyuni, Mjaka Haji Mjaka, alisisitiza kwa viongozi hao kubadilika kwa kuitisha vikao vya wanachama ili waweze kujua matatizo yanayowakabili wanachama wa jimbo lao.

Alifahamisha kuwa majukumu makubwa ya viongozi hao ni kuwalinda viongozi wao wakubwa, hivyo hawana budi kushirikiana nao ili waweze kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi wa jimbo Muyuni
pamoja na kuhakikisha jimbo hilo linapata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika kikao hicho wajumbe wa halmashauri kuu ya jimbo la Muyuni walijadili ajenda mbalimbali ikiwemo ya hali ya kisiasa kwa jimbo hilo, migogoro ya waananchi wa kijiji cha Jambiani ulipopatiwa suluhu hivi karibuni,

Mengine yaliyojadiliwa ni Rasimu juu ya uundwaji wa Katiba mpya kwa kuitolea maoni sahihi, pamoja na kutathmini chaguzi za chama pamoja na jumuiya zake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.