Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya printer ya rangi mshindi wa shindano la raffle Ndugu Gloria Agostina Mtemi lililoandaliwa na palm hotel ya pwani mchangani kusherehekea mwaka mpya wa 2012.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia mkono wafanyakazi wa Palm Hotel Ya Pwani Mchangani kama ishara ya kuwapongeza kwa kuchapa kazi vizuri na kuusherehekea mwaka mpya wa 2012.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Kitalii ya Palm iliyoko Pwani Mchangani Mkoa Kaskazini Unguja wamepongezwa kwa juhudi zao za kutoa huduma bora kwa wageni wanaotembelea Zanzibar Kiutalii.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Tafrija Maalum iliyoandaliwa na Uongozi wa Hoteli hiyo kwa Wafanyakazi wake ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2012.
Balozi Seif alikabidhi zawadi ya Printer ya rangi kwa Mshindi wa shindano Maalum Ndugu Goria Agostina Mtemi la kusherehekea mwaka mpya kwa Wafanyakazi hao lililopewa jina la Raffle
Alisema Watalii na Wageni wengi wamekuwa wakifurahia huduma nzuri zinazoendelea kutolewa kwenye mahotelini mbali mbali hapa Zanzibar.
Balozi Seif alisema ukarimu uliopo miongoni mwa wafanyakazi wa sekta hiyo ya Mahoteli unaashiria kuimarisha kwa sekta ya Utalii Nchini.
Tafrija hiyo Maalum iliyoandaliwa na Uongozi wa Hoteli ya Palm ya pwani Mchangani ilitoa fursa kwa wafanyakazi hao kula , kunywa na kufurahia pamoja mwaka mpya wa 2012.
Othman Khamis Ame
Ofisi yha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/1/2012.
No comments:
Post a Comment