Na Aboud Mahmoud
KAMPUNI ya Malik Food inayojishughulisha na biashara ya kuku, imetoa msaada wa mipira 100 kwa Jumuiya ya kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ), yenye thamani ya shilingi milioni nne.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Malik Faraji, amesema lengo kuu la kutoa msaada huo ni kusaidia vijana katika kuhakikisha wanajishirikisha katika michezo na kuachana na kujitumbukiza katika vikundi viovu.
Nae Katibu Mtendaji wa (COWPZ), Mgeni Hassan Juma, amehakikisha kuwa mipira hiyo itawafikia walengwa.
Aidha ameiomba kampuni hiyo kuendelea kutoa kuwasaidia vijana na wazazi katika kufanikisha upatikanaji wa maendeleo kimichezo na katika mambo mengine ya kijamii.
No comments:
Post a Comment