Na Mwajuma Juma
TIMU ya Kikwajuni iliyorudi ligi kuu ya soka Zanzibar msimu huu, imeendelea kutoa takrima baada ya juzi kuchapwa magoli 3-0 na Chipukizi katika uwanja wa Mao Dzedong.
Mabao yote ya washindi, yaliwekwa nyavuni na mchezaji Abdullatif Abdallah.
NAYE ABDI SULEIMAN, anaripoti kutoka Pemba kuwa, timu ya Ukombozi ya Kiuyu, inaendelea kubaki mkiani mwa ligi daraja la kwanza taifa baada ya kuchezea kipigo cha magoli 5-2 mikonini mwa wajenga uchumi, timu ya Duma katika dimba la Gombani.
No comments:
Post a Comment