Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mfereji kuangalia utokaji wa maji mara baada ya kufungua kisima cha maji katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipata maelezo kutoka kwa wajisiriamali huku akijiburudisha kwa chai, wakati akikagua bidhaa za wajasiriamali hao mara baada ya kuzindua mradi wa (MKUAJI) katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa (MKUAJI) katika shehia ya Mtoni Kidatu, Wilaya ya Magharibi Unguja. Kushotoni kwake (mwenye T-Shirt na kofia ya kapelo) ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Mhe. Nassor Ahmed Mazrui. (Picha, Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad (OMKR).
Na Hassan Hamad (OMKR).
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali inakabiliwa na changamoto kubwa ya kurekebisha mtaala wake wa elimu ili uende sambamba na mahitaji ya sasa ya kuwapatia vijana ajira mara wanapomaliza masomo yao.
Amesema zaidi ya vijana elfu moja na mia tano (1500) waliomaliza shahada ya kwanza na wengine kadhaa wa ngazi za diploma na cheti katika taaluma mbali mbali hawana ajira kutokana na mtaala uliopo kutowaandaa vizuri kuweza kujiajiri na kutegemea moja kwa moja ajira kutoka serikalini, hali inayojieleza wazi kuwa serikali haina uwezo wa kuwaajiri vijana wote katika kazi za maofisini.
Makamu wa Kwanza wa Rais ameeleza changamoto hiyo huko Mtoni Kidatu Wilaya ya Magharibi Unguja katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza Ujasiriamali na Ajira (MKUAJI) katika jimbo la Mtoni.
Amesema kufunguliwa kwa mradi huo kutaleta ukombozi wa kiuchumi na upungufu wa ajira kwa vijana wa eneo hilo, na kuomba majimbo mengine kufuata mfano huo ili waweze kuwakomboa wananchi wao na hali ngumu ya uchumi.
Amepongeza hatua ya kuanzishwa kwa mradi huo ambao utawasaidia wajasiriamali kwa kuwapatia ujuzi wa fani mbali mbali ambao utawawezesha kujiajiri na kuhimili ushindani katika soko la ajira.
“Vijana wetu bado hawana ujuzi wa kutosha, utaona katika makampuni makubwa ya kigeni yakiwemo mashirika ya ndege vijana kutoka nchi nyengine ikiwemo Kenya wanaonekana kufanya kazi, lakini vijana wetu wa Tanzania hasa Zanzibar hawamo kutokana na ujuzi mdogo wa lugha”, alitanabahisha Maalim Seif.
Katika hatua nyengine Makamu wa Kwanza wa Rais ametoa wito viongozi wa majimbo wakiwemo Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kushirikiana katika kutatua kero za wananchi.
Amewataka viongozi hao kujali maslahi ya watu na kuachana na tabia ya kuangalia maslahi huku akikumbusha kuwa “siasa ni utumishi wa umma na sio biashara wala maslahi binafsi”.
Amewaomba wadau wengine wa maendeleo zikiwemo taasisi binafsi kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana, na kwamba iwapo wataendelezwa tatizo hilo linaweza kumalizika.
Akizungumza katika hafla hiyo, muwezeshaji wa mradi huo bibi Lucy Mwaipopo amesema mradi huo wa miaka mitatu utakaotekelezwa kwa awamu mbili, utakuza ajira kwa vijana na kuhamasisha wajasiriamali kuweza kujikwamua na hali ngumu ya uchumi.
Amesema mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni na kituo cha mafunzo ya ujasiriamali Tanzania kanda ya Zanzibar, unakusudia kuanzisha benki ya vikundi kwa ajili ya wajasiriamali yaani Village Community Bank (VICOBA).
Amesema benki za aina hiyo zimeweza kuleta manufaa makubwa katika maeneo ya Tanzania Bara zilikoanzishwa, na kwamba kuwepo kwa benki hiyo kutaufanya mradi huo kuwa mfano katika kanda ya Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni ambaye ndiye mdau mkuu wa mradi huo Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui amesema mradi huo utajumuisha mafunzo ya fani mbali mbali na kulifanya eneo hilo kuwa kituo maalum cha taaluma kwa wajasiriamali.
Amesema iwapo viongozi wa majimbo mengine watakuwa na spidi kama anayoiendeleza katika jimbo lake, umaskini kwa wananchi unaweza kupungua kwa kipindi kifupi.
Zaidi ya shilingi milioni 32 tayari zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mradi huo kinachotarajiwa kikamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Uzinduzi wa mradi huo ulikwenda sambamba na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya uanzishaji wa mfuko wa mradi ambapo wadau mbali mbali walitoa michango yao ambapo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais iliahidi kuchangia shilingi milioni tatu na Mheshimiwa Mazrui aliahidi kuchangia shilingi milioni kumi.
Kabla ya uzinduzi wa mradi huo, Makamu wa Kwanza wa Rais alifungua rasmi kisima cha maji katika shehia ya Mtoni Kidatu, kinachotimiza idadi ya visima kumi na moja vilivyojengwa na Mhe. Mazrui katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Thats good idea and good perfomance .I advice all represenatives in our Provinces to be like this imean to pay more emphasis to the people from there provinces and not enriching them selves. God bless Zanzibar and their people .Amin
ReplyDeleteTatizo la vijana 1500 waliomaliza masomo ktk ngazi ya digirii kukosa ajira, linatokana na SMZ kupitia wizara yake ya elimu kusindwa kua na dira.
ReplyDeleteNchi zote duniani ktk mitaala yake, kutoa kipao mbele kwa zile sekta ambazo zinaajiri vijana kwa wingi lkn. kwa Z'bar ni tofauti.
Ukienda Uarabuni leo hii vijana wengi kule wamesomea fani ya jiolojia pamoja na fani nyingine zinazo husiana na hizo kwa vile shughuli kubwa kule ni uchimbaji wa mafuta.
Vile vile kwa nchi kama vile sychelles, nakumbuka hata Rais wao ALBERT REIN ALIKUA HOTEL MANAGER.
Lkn. hapa kwetu kila atasoma eidha ualimu au sheria. huwezi kukuta mwenye digrii ya hotel management au food production.
Mahotelini kule watu wanalipwa mamilioni ya shilingi.
Mimi nadhani wakati umefika kwa serikali, kuimarisha kile chuo cha maruhubi ili vijana wengi zaidi waweze kupata ajira huko.
Na pia wawaandae vijana kisaikolojia waamini kua kufanya kazi hoteli sio uhuni na badala yake ni kazi kama zilivyo nyingine na hii pia itapunguza manung'uniko kwamba ajira hizo zinachukuliwa na wageni