Na Mwashamba Juma
MWENYEKITI wa ZAYEDESA, Mama Shadiya Karume amekabidhi serikalini nyumba ya kulelea watoto iliyopo Mazizini wilaya ya Magharibi Unguja, iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 60 katika ujenzi wake.
Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za ZAYEDESA, Mazizini kwenye hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makabidhiano ya jengo hilo kati ya katibu wa ZAYEDESA, Lucy Majaaliwa na Katibu Mkuu wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Fatma Gharib Bilal.
Katika hafla hiyo Mama Shadya alisema kukabidhi jengo hilo kwa serikali kumetimiza haki ya kisheria, licha ya kupambana na changamoto za hapa na pale wakati wa kujengwa kwake hatimae kumalizika na kulikabidhi mikononi mwa serikali.
Alisema kujengwa kwa nyumba hiyo kunafuatia kuchakaa kwa nyumba ya zamani iliyokuwa Forodhani, iliyotolewa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 chini ya uongozi wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume.
Alifahamisha kwamba watoto wanahitaji huduma zote za msingi za kijamii zikiwemo makaazi, malezi bora na huduma nyengine kama vile elimu, mavazi na chakula.
Alisema ni imani na mapenzi aliyonayo kwa watoto hao, ndipo alipoona upo umuhimu wa kujengewa nyumba mpya na ya kisasa.
Aidha aliwaomba walezi wa watoto hao kuzidisha mapenzi na imani na kuwa na mashirikiano na wizara husika katika kuwalea watoto hao ili wajihisi kama watoto wengine katika jamii.
Kwa upande wake waziri wa wizara hiyo, Zainab Omar Mohammed alisema kitendo cha utiaji saini wa mkataba huo kinaweka bayana majukumu ya kila upande kuendeleza nyumba hiyo kwa manufaa na faida ya watoto hao na taifa kwa ujumla.
Alisema fikra za mama Shadya za kuwasaidia na kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi watoto yatima zinakwenda sambamba na zile za Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abied Amani Karume.
Alisema wizara yake itaendeleza mashirikiano mazuri yaiyopo na ZAYEDESA, ambayo ndiyo iliyojenga nyumba hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Mama Shadya Karume.
Nyumba hiyo ya kulelea watoto yatima ya Mazizi ilifunguliwa Agosti 28 mwaka 2010 ambayo inaendeleza majukumu yake ya kulelea watoto hao kufuatia kuhama nyumba kongwe iliyochakaa ya Forodhani.
Mh hapa we acha tu. kama kuchaa mbona imeweza kutengezwa mikahawa. restaurant tofauti. hii sababu haina msingi itafutwe nyengine.
ReplyDeleteSababu ni njema, haina dosari wala isiwe sababu mapetengezwa nn pale forodhani. Jitihada kaonesha lazima apewe shukrani yk.
ReplyDeleteKawaida sisi huwa hatujuwi mabadiliko ya nyakati yakitoke hungangania tulichorithi.
Mimi sipo Zanzibar lakini hii nyumba ya Forodhani naijuwa vyema tokea hapo ilipokuwa Muslim Academy.
ReplyDeleteIwapo imetolewa fidia sioni kama ni tatizo hassa ikiwa ni kitu kipya almuraddi iwe inakidhi haja na pia itapunguza mazigo wa gharama za matengenezo.Nakubaliana na mtoa maoni alotangulia kuwa lazima twende na wakati na kukubali mabadiliko.
Ni jambo jema, kimsingi yale mazingira hayakua sahihi mazuri tena kwa watoto, kwa kweli mimi nafurahishwa sana na 'project' za namna hii kwa vile zinasaidia kuufanya mji mkongwe kua wa kitalii zaidi kwa kupunguza shughuli za kiserikali katikati ya mji.
ReplyDelete