Habari za Punde

Mahafali ya Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Haji Omar Kheir akihutubia katika mahafali ya nne ya Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA) kulia Mkurugenzi wa chuo hicho,Harusi Masheko na Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Abdalla Suleiman sherehe hizo zlifanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari mjini Unguja
Nada Ali Khamis (kushoto) mhitimu wa Diploma ya Rasilimali Watu katika Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA)akipokea zawadi maalum kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri muda mfupi baada ya kuwatunuku Stashahada wahitimu wa kada mbali mbali katika sherehe za  mahafali ya nne ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya wizara ya Habari kikwajuni mjini Zanzibar juzi , Nada ambaye ni mlemavu wa viungo anajishughulisha na biashara ndogo ndogo.kulia Mkurugenzi wa IPA, Harusi Masheko
 VIONGOZI na waalikwa mbali mbali wakishuhudia sherehe za mahafali ya nne ya Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA) zilizofanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari mjini Zanzibar jana
WAHITIMU mbali mbali wa Chuo cha utumishi wa Umma Zanzibar (IPA) wakiwa katika sherehe za mahafali ya nne ya chuo hicho zilizofanyika katika viwanya vya Wizara ya Habari jana

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Haji Omar Kheir akimtunuku zawadi mwanafunzi bora wa Diploma ya Rasilimali Watu katika chuo cha utumishi wa umma Zanzibar (IPA),Said Mbarouk katika sherehe za mahafali ya nne ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari mjini Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Haji Omar Kheir akimtunuku zawadi mwanafunzi bora wa Diploma ya Uongozi wa Umma katika chuo cha utumishi wa umma Zanzibar (IPA),Salha Mansour katika sherehe za mahafali ya nne ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari mjini Zanzibar.



1 comment:

  1. mkuu tunaomba maelezo yaendane na picha,maana hatujapata hint yoyote ktk hizi picha

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.