Na Hafsa Golo
WANAWAKE wajawazito wameshauriwa kufika hospitali mapema wanapojisikia kuanza kuumwa ili kuondosha usumbufu na matatizo wakati wa kujifungua.
Ushauri huo umetolewa na Ofisa mmoja wa ngazi za juu wa Hospitali ya Mnazimmoja ambae hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Ofisa huyo alilazimkia kutoa ushauri huo baada ya mama mmoja kujifungua nje ya hospitali ya wazazi ya Mwembe Landu, kwa kile kinachodaiwa kukosa huduma.
Alisema kuwa katika kitengo anachofanyia kazi, hawajapokea malalamiko yoyote, kutoka mwananchi huyo, hivyo hawataweza kuchukuwa hatua yoyote.
Alisema ni vyema kinamama wajawazito kufuata tarehe wanazopangiwa ma madaktari za kujifungua na waweze kufanya maandalizi mapema ya kufika hospitali na sio kuwabebesha lawama wauguzi jambo ambalo wakati mwengine kinimama wajawazito ndio wanaochangia kutokea kwa matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa mapema.
Kauli ya ofisa huyo imekuja baada ya kuwepo taarifa za mwwanamke mmoja kujifungua nje ya hospitali ya Muembe ladu lakini akakosa kuhudumiwa na wauguzi wa hapo bila kueleza sababu za kimsingi za kuchukua uamuzi huo.
Sakata hilo bado linaendelea kwa vile kumejitokeza kauli tafauti Zinazopingana na maelezo ya awali yaliotolewa na mlalamikaji na jamaa zake.
Alisema siku zote mama wajawazito hupewa elimu ya kufika hospitali mapema mara tu wanapohisi dalili za kuumwa na uchungu ili kuepusha matatizo ya aina hiyo.
Akizungumzia suala la kutozwa pesa kwa wajawazito alisema sio haki na anaestahiki kutoa pesa ni yule ambae anahitaji kufanyiwa upasuaji, hivyo amewataka wananchi kutokubali kutoa pesa kwani kufanya hivyo ni kuchangia rushwa.
Ofisa huyo akizungumzia mkasa wa mwanamke anayedaiwa kujifungulia nje ya hospitali, alisema anasikitishwa na yaliyompata mwanamke huyo, Mgomvi Abdalla (36)
Mama huyo alisema baada ya kushindwa kuingia hospitalini humo, alimtuma mtoto wake, Khamis Mussa 17, ili kwenda kuwaita wauguzi lakini walishindwa kufika kwa muda huo.
Hata hivyo, alisema alishangazwa sana kudaiwa shilingi 8000 na wauguzi hao wakati walishindwa kumpatia hata huduma ya kuzalishwa.
"Nimeshangazwa sana na kunidai shilingi 8000 na nimeenda na vifaa vyote ila sindano wakasema niwapatie pesa hizo kwa ajili ya sindano"alisema mama.
Alisema baada ya kujifungua na dereva wa gari aliokuwa kapanda kufanya fujo ndipo akateremka muhudumu kwa kumpeleka ndani ya hospitali.
No comments:
Post a Comment