Habari za Punde

Kisena Awafumba Mdomo Wabunge wa Jiji

Ataka UDA isifanywe siasa

Na Kunze Mswanyama

WABUNGE wa mkoa wa Dar es Salaam, wametakiwa kuacha siasa katika kulijadili sakata linalolikabili la shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA), huku wakipoteza muda mwingi ambao hauna manufaa kwa wapiga kura wao.

Mgogoro huo ambao umekuwa kama mchezo wa kuigiza unamuhusisha Meya wa Jiji la Dar es Salaam na kampuni ya Simon Group Limited, huku wabunge wa jijini wakihoji masuala mazima ya uuzwaji wa shirika hilo.


Mmiliki wa UDA, Robert Kisena aliwaeleza waandishi wa habari kuwa sakata hilo linakuzwa na mfanyabiashara mmoja kijana ambaye haijulikani amepata wapi mamlaka ya kuihoji serikali impatie nyaraka za uuzwaji wa UDA kwa kampuni ya Simon Group Limited.

Kisena alisema haoni kama kuna suala kubwa kwenye sakata hilo, ila kilichopo ni wabunge wa jijini kulikuza kiasi ambacho kimekuwa kikizorotesha shughuli za maendeleo katika mkoa huo.

Kisena alisema si jukumu lao kujua kwanini alinyimwa wala alikuwa wangapi kuomba tenda ya kulinunua shirika hilo.

Kisena alisema sakata la UDA limegeuzwa ulingo wa mivutano kisiasa baina ya Meya wa Jiji na baadhi ya Wabunge wa jiji ambao wanahisi Manji kuwa ndiye mtu sasahihi wa kupata tenda hiyo na sio Simon Group Limited.

Alisema wabunge hao wanashindwa kuelewa adha ya usafiri wanayokumbana nayo wanafunzi wanaosoma katika skuli mbalimbali katika jiji hili hususan wakati wa kwenda na kutoka skuli.

Alisema Jiji hilo linakabiliwa na matatizo mengi yanayo hitaji kufanyiwa kazi, matatizo kama huduma za afya, matatizo yasiyoisha kwenye skuli, maji,umeme na tatizo la usafiri wenyewe yote haya bado ni shubiri katika jiji hili yaliyo kosa majibu ya maana.

Aliwataka wabunge hao kutotumia muda wingi katika kuhadili suali la UDA bali washiriki katika kupunguza matatizo ya wananchi na kwamba kushughulikia matatizo ya wananchi ndio kumsaidia Rais katika kuhakikisha kila Mtanzania anaondokana na umasikini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.