Mama Asha Suleiman Iddi Mke wa Balozi Seif akisalimiana na wana CCM wa Tawi la Wesha kwenye Mkutano wa Hadhara mara baada ya uwekwaji wa jiwe la msingi la Tawi hilo.
Wana CCM wa Tawi la Wesha wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani mara baada ya kuweka jewel la masingi la tawi hilo.
Wakati umefika kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Nchini Kuhakikisha kwamba Viongozi wenye kugugumizi cha kutekeleza Sera na Ilani ya Chama hicho hawapatiwi fursa tena ya kukiongoza Chama chao.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alioa tahadhari hiyo wakati akizungumza na baadhi ya Wanachama wa CCM kwenye mikutano tofauti baada ya kufanya kazi za chama kwa kuweka mawe ya msingi ya matawi ya Mbuzini na Wesha katika Mikoa miwili ya Pemba.
Balozi Seif akiwa pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ushindi wa CCM kuendelea kuongoza Taifa la Tanzania utaimarika zaidi iwapo Wanachama hao watawatenga Viongozi hao. “ Tafadhalini msikubali kuingiza Virusi ndani ya Chama cha Mapinduzi kwa kufanya hivyo ni hatari ambayo wanaweza kuja ijutia”
Alitahadharisha Balozi Seif. Amewakumbusha Viongozi wa CCM kutangaza Maendeleo yaliyopatikana Nchini ambayo yametokana na Sera za Chama hicho baada ya kupata ridhaa ya Wananchi katika uchaguzi Mkuu uliopita.
Alisema CCM imewafanyia mengi Wananchi licha ya baadhi ya Watu kujifanya hayaoni .Hivyo kwa mtazamo huo ipo haja kwa Viongozi wa CCM kuendelea kuwaelimisha Wananchi pamoj na watu hao. “ Inasikitisha kuona Baadhi ya watu wanafikia hatua ya kuwadanganya Wananchi mchana bila ya kuona haya.
Watu hao wanafaa kuzomewa na kuepukwa” Alitahadharisha Mjumbe huyo wa Kamamati Kuu ya CCM. Balozi Seif aliwapongeza Viongozi na Wanachama Kisiwani Pemba kwa umahiri wao wakukiongezea wanachama chama hicho ambapo tafiti zinaonyesha idadi ya wanachama wake inaongezeka siku hadi siku. “
Kura za Wana CCM Kisiwani Pemba ni muhimu kwa Ushindi wa Chama hicho katika Chaguzi mbali mbali Nchini”. Alifafanua Balozi Seif Ali Iddi. Alisisitiza kwamba Chama cha Mapinduzi bado kinapendwa na Wananchi wengi Nchini cha msingi ni Wanachama wenyewe kujipanga vizuri katika kuwahudumia vyema Wananchi wote.
Balozi Seif aliwahimiza Wana CCM hao kuendelea zaidi kujenga Matawi bora na ya kisasa yenye hadhi ya Chama hicho. Ndani ya ziara hiyo ya kutembelea na kuzungumza na Wana CCM NDANI YA mikoa miwili ya Pemba Balozi Seif aliahidi kusaidia Ujenzi wa Tawi la CCM la Kijiji cha Kiuyu mara baada ya
Wanachama hao kuanza kazi za Ujenzi wa Msingi. Balozi Seif pia akaahidi kuchangia Mabati yote kwa ajili ya uwezekaji wa Matawi ya CCM ya Vijiji vya Mbuzini na Wesha Chake chake. Katika Risala zao Tofauti
Wana CCM wa Matawi mbali mbali aliyoyatembelea Balozi Seif wameahidi kutekeleza vyema Sera za Chama cha Maapinduzi katika Utoaji wa maoni katika mchakato wa Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati utakapofika.
Wanachama hao pia wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuongeza bei zao la karafuu llilopelekea wananchi wengi kuneemeka na kunyanyua vipato vyao.
Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu w Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment