Na Ameir Khalid
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka Zanzibar timu ya Mafunzo, jana ililazimika kugawna pointi na Super Falcon baada ya kwenda sare isiyokuwa na magoli.
Pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Mao Dzedong, lilikuwa kali na la kuvutia huku wachezaji wa timu hizo wakihaha uwanja mzima kusaka mabao.
Hata hivyo milango ya timu hizo ilikuwa migumu, ambapo magolikipa walikuwa makini kluokoa mashambulizi kadhaa waliyoelekezewa.
Sare hiyo imeifanya Super Falcon inayoshika usukani wa ligi hiyo kuifiklsha pointi 30 kutokana na michezo 18, wakati walinda wafungwa wa Kinua miguu wana akiba ya pointi 26 baada ya kucheza mechi 17, wakiwa katika nafasi ya nne.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo uwanjani hapo, ambapo Miembeni United itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya makamu bingwa msumu huu, timu ya Jamhuri.
No comments:
Post a Comment