Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa uokozi na kuepuka Majanga Nchini Israel Bwana Gideon Kader kwenye Hoteli ya David Ciladel Mjini Jerusalem. Kushoo mwa Balozi Seif ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd na Kulia ni Balozi wa Israel Kenya na Tanzania Bwana Kasbia Niruel Chirich.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifahamishwa hatua za mfumo unaochukuliwa wa kukabiliana na Maafa katika Miji ya Israel unaotumia Mtandao wa Kisasa. Nyuma ya Balozi ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Bwana Ali Juma Hamad.
Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Raia Nchini Israel { Home Front Command } Luteni Kanal Tai Peleg akitoa darasa kwa Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif namna ya kukabiliana na Maafa
Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa Uokozi pamoja na kuepuka Majanga Nchini Israel inaangalia uwezekano wa namna ya kuisaidia Zanzibar katika harakati zake za kupambana na Maafa wakati yanapotokezea Maafa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bwana Gedion Kandel wakati wa mazungumao yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yupo Nchini humo kwa ziara ya Kiserikali mazungumzo yaliyofanyika hapo katika Hoteli ya David Citadel Mjini Jerusalem.
Bwana Gedio alisema Taasisi yake tayari imeyapokea maombi ya Zanzibar na kukubali kushirikiana pamoja wakati yanapotokezea matatizo ya Majanga na hatimaye kupelekea Maafa . Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Utafiti,Uchunguzi na uokozi pamoja na kuepuka Majanga aliishauri Zanzibar kuandaa Mpango Maalum wa maeneo ambayo Taasisi yake inaweza kusaidia.
Alisisitiza kwamba vitengo vya Maafa hufanikiwa vyema katika utekelezaji wa majuku yake endapo Bajeti ya Vitengo hivyo inakuwa ya kuridhisha.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pia aliiomba Taasisi hiyo kusaidia mafunzo kwa watendaji wa Kitengo cha Maafa Zanzibar ili kiwe na uwezo zaidi ya Kitaalamu.
Balozi Seif alisema Majanga yanayopelekea kutokea kwa Maafa yanaweza kupungua kutokana na uwajibikaji mkubwa wa watendaji hao unaoambatana na Taaluma ya kina. Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake alitembelea Taasisi ya Usalama wa Raia inayojishughulisha na Maajanga Home Front Command { HFC } Mjini Telaviv.
Mkuu wa Taasisi hiyo Luteni Kanal Tai Peleg aliueleza Ujumbe wa Zanzinbar kwamba Taasisi hiyo imeundwa kufuatia Janga la Maafa yaliyokuwa ayakiikumba Nchi hiyo likiwemo lile la Mashambulizi ya Kivita.
Alisema Taasisi hiyo tayari imejijengea umaarufu mkubwa kutokana na watendaji wake kushiriki katika kutoa msaada wa Kiufundi kwenye Matukio ya Maafa mbali mbali Duniani.
Ameishauri Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla kutumia fursa ya mafunzo yatakayotolewa na Taasisi hiyo katika Semina itakayofanyika mnamo mwezi wa Septemba mwaka huu wa 2012.
No comments:
Post a Comment