Habari za Punde

Mwizi Anapokimbilia Msikitni



Nikiwa katika Daladala maeneo ya sogea nilikutana`na mkasa wa aina yake pale ambapo kuna mtu alinadiwa mwizi na katika kusalimisha usalama wake aliona bora akimbilie Msikitini na kujifungia  ndani.

Nikiwasikiliza abiria waliopo kwenye dala dala wakisimulia kisa na mkasa wa  mwizi huyu na wengine ambao hutafuta himaya ndani ya nyumba za ibada kulikuwa na riwaya tofauti za jinsi mwizi ambaye pengine hata kusali hasali lakini mambo yanapomzidia anajua kwamba Waislamu wanaziheshimu nyumba za Ibada na hivyo akiwepo humo basi yuko “salama” na maisha yake angalau kwa muda mpaka wafike wanausalama kumshughulikia.


Msikiti ni nyumba ya ibada kwa waumini wa dini ya kiislamu. Si ibada pekee inayofanyika hapo bali pia ni nyumba ya utulivu, husomeshwa darsa na mafundisho ndani yake, husaliwa,  hufanywa dhikr  na mengi mengineyo.

Ni nyumba ambayo kila anaeingia ndani hupaswa kuwa katika hali ya utulivu bila ya kushughulisha au kuwabughudhi wengine walio kwenye ibada tofauti sasa akiingia mwizi katika hali hii sijui msikitini itakuwaje.
Tasawwar Waislamu wanasali Jamaa Msikitini wakitekeleza Sala ya fardhi na ghafla mwizi aingie humo kujisalimisha nafsi yake kukimbia kipigo  ambacho laiti asingekimbilia Msikitini kingeweza kusababisha mauti yake.

Je Waumini Wanaosali unadhani watafanya kitu gani ilhali tayari wameghulishwa katika sala zao? 

1 comment:

  1. tunavoambiwa tusiwache swala ya fardhi kwa kitu chochote

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.