Habari za Punde

Ngorongoro Heroes Yaifuata Sudan Leo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', kinatarajia kuondoka leo kwenda Sudan kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Sudan itakayochezwa Mei 5, mwaka huu.

Msafara wa Ngorongoro Heroes utakaokuwa na watu 28 ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF', Athuman Kambi, umepangiwa kuondoka saa 8.45 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.


Ngorongoro Heroes itaagwa rasmi kwa kukabidhiwa bendera ya Taifa mnamo saa 5:00 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Wengine katika msafara huo ni wachezaji na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Kim Poulsen.

Mechi hiyo ya marudiano namba 16 ya kuwania kufuzu michezo ya Olimpiki itakayofanyika London Uingereza mwezi Juni, itachezwa kwenye uUwanja wa Khartoum kuanzia saa mbili usiku kwa saa za Sudan.

Iwapo Ngorongoro Heroes ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 3-1 itafanikiwa kuitoa Sudan, itapambana na Nigeria ambayo yenyewe imefuzu moja kwa moja kucheza raundi ya pili ya michuano hiyo.

Mechi ya kwanza itachezwa Julai 28 jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika Nigeria kati ya Agosti 10, 11 na 12 mwaka huu, ambapo fainali za U-20 kwa Afrika zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.